Barcelona,Celta de vigo watinga nusu fainali

Mabingwa watetezi wa kombe la Mfalme Barcelona wamesonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Barcelona waliwachapa Athletic Bilbao kwa mabao 3-1 yalitiwa kimyani na Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymer na hivyo barca kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2.

Nao Celta de vigo waliwaondoa katika michuano hiyo vijana wa Diego Simione Atletico Madrid kwa kuwachapa kwa mabao 3-2.

Robo fainali ya pili itapigwa leo usiku kwa Las Palmas kushuka dimbani kuwakabili Valencia, huku Mirandés wakiwa na kibarua pevu dhidi ya Sevilla.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments