AU yasifia Rwanda kurahisishia wageni kupata VISA.

Katika mkutano unaojumuisha mawaziri wa ushirikiano wa kimataifa katika jumuiya ya EAC ambao unaendelea mjini Adiss Ababa nchini Ethiopia , Rwanda imepongezwa kutoa mfano mzuri wa kurahisishia wafanya biashara katika nchi za Afrika.

Katika mkutano huo Rwanda inawakirishwa na waziri wa mambo ya nchi za nje Bi Louise Mushikiwabo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Waziri Mushikiwabo amesema kuwa hii ni sera ya Rwanda ya kutowa VISA ukiwa ni mfumo wa kurahisishia wafanya biashara katika nchi za Afrika.

Dr.Nkosazana Dlamini Zuma Kamishna mkuu wa Umoja wa Afrika AU alisema kuwa mataifa yote yanapaswa kushirikiana ili kujenga mwelekeo wa 2063.

Aidha Bi Zuma amewaomba waafrika kujenga bara la Afrika lenye Usalama na amani na kuwa mfano bora katika dunia nzima.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments