Rwanda kwenye nafasi ya 4 barani muri Afrika kupambana na rushwa

Ripoti ya shirika la kupambana na rushwa (Transparency International) leo jumatano tarehe 27 januari 2016, imetangaza kwamba Rwanda imewekwa kwenye nafasi ya 4 kama nchi iliyopunguza rushwa barani Afrika na ya kwanza katika jumiya ya Afrika ya mashariki.

Rwanda imewekwa kwenye nafasi ya 44 duniani. Ripoti hii pia inaonyesha kuwa mataifa yenye usalama mdogo kunaripotiwa rushwa zaidi kuliko mataifa mengine.
Mataifa yanayoripotiwa kuwepo rushwa nyingi ni Angola, Sudan ya kusini, Afghanistan, Korea ya Kaskazini, Guinea Bisau , Somalia….

Danmark ndilo taifa ambalo limeripotiwa kuongoza kwa mataifa duniani ambako rushwa ni ndogo na alama 91 % , mwaka uliopita wa 2014 nchi hiyo ilikuwa ikiongoza na alama 92%.

Barani Afrika, Rwanda inashikilia nafasi ya 4 na alama 54% baada ya Botswana, Capverde na Ushelisheli. Ukilinganisha na mwaka uliopita 2014, imeearifiwa kuwa Rwanda imefanya vizuri ikiwa na alama tano kwani ilikuwa na alama 49.
Kiongozi wa Transparency International Rwanda Bi Ingabire Marie Immaculee, hajaridhishwa na nafasi Rwanda iliyopo hivi sasa , anawaasa wanyarwanda kupiga hatua zaidi kupambana na rushwa.

Katika eneo la Afrika ya mashariki Tanzania ni nchi inayoshikilia nafasi ya 2 kupambana na rushwa na nafasi ya 117 duniani, Kenya kwenye nafasi ya 139 duniani sawa na Uganda. Burundi inakuja kwenye nafasi ya 159.

Utafiti huu umefanywa katika mataifa 169 duniani.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments