CHAN 2016 : ¼ Fainali kati ya Rwanda na DRC ni kivumbi na jasho

Rwanda vs Congo 1/4 CHAN 2016

Rwanda itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika robo fainali ya michuano ya soka barani Afrika kuwania taji la CHAN 2016 kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Mchuano baina ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambao umepangwa kuchezwa jumamosi umekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na katika mitaa ya jiji la Kigali kwa jumla.

Rwanda ilifuzu baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi la A kwa alama 6, mbele ya Ivory Coast ambayo pia ilifuzu ikiwa pia na alama 6 lakini kwa uchache wa mabao kwa timu hizo mbili .

Kwa mujibu wa sheria za CAF timu zikitoka sare wanaangalia mchezo uliiozikutanisha ikiwa moja iliyoshinda nyingine halafu inatawazwa mshindi wa kwanza halafu nyingine inachukua nafasi ya pili.

Mchuano wa DRC na Rwanda, utapigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali na ni mchuano ambao unatarajiwa kuzua hisia kubwa baina ya mashabiki wa nchi zote mbili.

Uwanja wa Amahoro unatarajiwa kufurika kwa maelfu ya mashabiki na licha ya Rwanda kuwa nyumbani mashabiki wa DRC wanatarajiwa kuvuka mpaka kuishangilia Leopard.

Mashabiki wa timu zote mbili walitamani sana mataifa hayo jirani yangekutana katika fainali ya taji hilo na kombe hilo kubaki katika eneo la Afrika ya Kati, lakini hili halijatimia.

Mara ya mwisho kwa mataifa haya yote kukutana ilikuwa ni mapema mwezi huu katika mchezo wa kirafiki kabla ya kuanza kwa michuano hii na Rwanda waliifunga DRC bao 1 kwa 0.

Cameroon nayo itakabiliana na Ivory Coast katika robo fainali nyingine pia siku ya Jumamosi katika uwanja wa Huye mjini Butare.

Timu ya Cameroon ilifuzu baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi B kwa 7 mbele ya DRC, huku Ivory Coast ikimaliza ya pili katika kundi A kwa alama 6.

Mwaka 2004, wakati Rwanda iliposhiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya kombe la soka la mataifa barani Afrika CAN, ilikuwa kwenye kundi moja na DRC, katika mchuano wao Rwanda iliilaza kwa bao 1-0 lililofungwa na Said Abed Makasi
mkongomani akiwa na urai wa Rwanda. Baada ya kukandikwa bao hilo, kutokana na kupandwa na hasira nyumba ya wazazi wake ilichomwa moto mjini Bukavu wakidai kwamba ndugu yao kawanyima raha.

Mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana, ilikuwa ni mwaka 2015 katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika, mchuano ambao Ivory Coast waliishinda Cameroon bao 1 kwa 0.

Kiingilio katika mechi ya Rwanda na DRC kwenye uwanja wa taifa wa Amahoro nafasi za kawaida, ilikuwa ni faranga 500 sasa tikikiti imepanda hadi 1000 Frs. Nafasi ya franga 2000 imepanda hadi franga elfu 4 za Rwanda karibu ya jukwaa la heshima ni 10.000 Frs na kwenye jukwaa la heshima ni 20.000 Frs.

Leopard imeshiriki katika makala yote ya CHAN tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 nchini Côte d’Ivoire, mwaka ambao waliibuka mabingwa wa kwanza wa taji hili.
Kocha Florent Ibenge wa DR Kongo mapema alisema anafahamu kuwa kundi la B lilikuwa gumu lakini, vijana wake wamejiandaa na wana uwezo wa kunyakua ubingwa wa mwaka huu.

Mechi hiyo inatazamiwa na wengi ni ile kati ya DRC dhidi ya Amavubi ya Rwanda. Siku hiyo ya Jumamosi tarehe 30 januari itakuwa pia ni siku ya shughuli za pamoja maarufu Umuganda.

Mwishoni mwa juma lililopita, Leopard ilifungwa na Amavubi Stars ya Rwanda bao 1 kwa 0 kwenye uwanja wa umuganda, mjini Gisenyi katika mchuano wa kirafiki kwa maandalizi ya michuano hii.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments