Rwanda yapata marubani wa ndege 9 wapya


Wanyarwanda 9 wakiwemo wasichana 3 wamehitimisha mafunzo ya kuwa marubani wa ndege nchini Ethiopia. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 26 January 2016 nchini Ethiopia.

Akiongea na Igihe.com, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Rwandair, bwana Mirenge John amesema kuwa yale wanayojivunia ni pamoja na watoto wa kinyarwanda waliosaidiwa kujifunza kuwa marubani wa ndege.

Mirenge John ameongeza kuwa hivi sasa Rwanda ina marubani 18 na wengine 16 siku za hivi karibuni watakuwa wamehitimisha masomo yao.

Aidha, Rwanda ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya kusajili marubani wa ndege kutoka mataifa mengine na kusababisha kuigharimu pesa nyingi Kampuni hiyo ya Rwanda Air.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments