CHAN 2016 :Nigeria yashindwa kufuzu ¼ fainali

Bao la Guinea likitingwa nyavuni na Ibrahima Sankhon

Guinea 1 - 0 Nigeria

Niger 0 - 5 Tunisia

Mashindano ya kuwania kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN yanaendelea kutimua vumbi nchini Rwanda, katika kundi C , Nigeria wamepokonywa bao 1-0 na Guenea katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Umuganda huku Niger wakinyeshewa mvua ya magoli 5-0 na Tunis katika uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Kikosi cha Nigeria

Guenea na Tunisia wamekata tikiti ya ¼ fainali ya CHAN 2016. Bao pekee la Guenea limepachikwa wavuni katika dakika ya 45 na Ibrahima Sankhon,

Ibrahima Sankhon

Katika kundi hilo la C, mabao ya Tunisia yamewekwa kimyani na Saad Bguir amefunga mabao mawili , dakika ya 5 na 39, Ahmed Akaichi katika dakika ya 79 Mohamed Ben Amor akapachika kunako dakika ya 81 na Hichem Essifi dakika ya 90.


wachezaji wa Tunisia wakifurahia ushindi
.
Mechi za kundi C, zimechezwa kwa wakati mmoja, ila viwanja tofauti.

Michuano ya kundi D imepangwa kuchezwa jumatano wiki hii ambapo Uganda itamenyana na Zimbabwe na Zambia itamaliza kazi na Mali.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments