Nigeria na Tunisia zatoka sare ya kufungana 1-1


Ahmed Akaichi aliyeifungia Tunisia mabao mawili katika mchuano wake na Guinea katika michuano ya CHAN, leo ameandika bao la tatu dhidi ya Nigeria.

Tunisia 1 : 1 Nigeria

Niger 18:00 Guinea

Timu ya taifa ya soka ya Tunisia inayoshiriki katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ya nyumbani CHAN inayoendelea nchini Rwanda, imetoka nyuma na kusawazisha bao walilokuwa wamefungwa na Nigeria katika mchuano wa kundi C.

Mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali umemalizika kwa timu zote mbili kufungana bao 1 kwa 1.

Timu ya Nigeria

Bao la Nigeria limefungwa na chisom Chikatara kunako dakika ya 53 ya mchezo na baadae Ahmed Akaïchi akasawazisha bao hilo katika dakika ya 70.

Karenzi Christopher

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments