CHAN 2016 : Balaa katika uwanja wa Huye giza kutanda dakika 12

Giza lilitanda uwanjani

Huku mashindano yakiendelea ya CHAN katika kundi B mjini Huye katika mkoa wa kusini mwa Rwanda, giza lilitanda uwanjanani kwa muda wa dakika 12 baada ya kukosekana kwa umeme wakati timu ya Cameroon Simba wa nyika na Ethiopia zilipokuwa zikimenyana.

Habari ambazo zimefika makuruki.rw, ni kwamba tatizo hilo lilitokana na uhaba wa mafuta kwenye engine ambapo wafanyakazi wawili wa MINISPOC akiwemo Aimable Sebadari wanatuhumiwa kutowajibika kufanya kazi ipasavyo, baada ya kuokea tatizo hilo wamewekwa ndani kujieleza.

Giza lilitanda katika uwanja wa soka wa Huye

Baadhi ya maafisa wanaohusika na mashindano ya CHAN walitoka nje kuchunguza balaa hilo lililotokea akiwemo waziri wa michezo na utamaduni Uwacu Julienne.

Imearifiwa kwamba kwa msaada wa kijeshi, mafuta yaliletwa haraka hadi kwenye uwanja wa Huye.

Umeme ulirejea baada ya dakika 12, wachezaji wakaendelea mtanange wao, baada dakika chache kipindi cha kwanza kilimalizika.

Baada ya kurejea umeme uwanjani, shirikisho la soka barani Afrika ( CAF), kupitia tweeter, waliandika eti : Tumerejea baada ya umeme kupotea katika uwanja wa Huye’’ Matokeo yalikuwa Cameroon 0-0 Ethiopia.

Balaa kama hili liliwahi kutokea barani Afrika tarehe 08 septemba 2015 nchini Zambia katika uwanja wa Heroes, kulikuwa na mpambano wa kimataifa kati ya Zambia na Gabon, wakati huo kulikosekana umeme.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments