Mataifa tajili duniani G20 yanakabiliana na kilimo

Watafiti wapatao 100 kutoka mataifa 8 wako katika mkutano nchini Rwanda unaojadili kuhusu kilimo cha kisasa hususani katika mataifa yaliyokwisha piga hatuwa.

Waziri wakilimo wa Rwanda bi Gerardine Mukeshimana amesema kuwa kilimo chahivi sasa kimebadilika kutokana na kubadilika kwa nyakati. Kwamantiki hiyo kunahitajika jibu sahihi kwa wakurima wa kisasa.

Musimamizi wa shilika la chakula duniani "FAO" nchini Rwanda bwana Attaher Maiga, amesema kuwa mradi huu ulianzishwa katika mataifa 8 na Rwanda ikiwemo.

Kwa mujibu wa gazeti Izuba rirashe Bwana Maiga ameongeza kuwa mwelekeo wa Rwanda ni mzuri katika mabadiliko ya kilimo.

Maiga ametaja kuwa takwimu duniani zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 800 wana uhaba wa chakula, lakini cha kujivunia ni kwamba idadi hiyo imeanza kupungua.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments