CHAN 2016 Zambia yaibwaga Zimbabwe 1-0

Zambia yawika Rubavu

Mashindano ya CHAN yameingia siku yake ya nne nchini Rwanda, jumanne ya tarehe 19 januari,Timu ya taifa ya Zimbabwe na Zambia zilizopo kwenye kundi D zimeshuka dimbani wilayani Rubavu mjini Gisenyi katika jimbo la Magharibi.
Zambia imewachapa majirani zao Zimbabwe bao moja kwa nunge.

Zimbabwe imetawala uwanja katika kipindi cha kwanza, baada ya mapumziko, timu ya Zambia Chipolopolo wamebadili mchezo na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Zambia imefanikiwa kuandika bao katika dakika ya 57 likifungwa na Isaac Chansa baada ya kupokea krosi kutoka kwa nahodha wao Christopher Katongo.

Katonge aliyevaa jezi ya kijani ndiye ametoa pasi iliyemfikia Chansa naye bila kusimamisha akaachia mkwaju litalinga bao

Hadi kipenga cha mwisho kupulizwa, Zambia imetoroka na ushindi wa bao 1-0.


Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments