FRODEBU yasema mazungumzo ya amani muhimu

Mazungumzo ya Amani yaliyopangwa kufanyika tena Januari 6 mjini Arusha, Tanzania.

Kiongozi aliye uhamishoni wa chama cha Opposition Front for Democracy in Burundi amesema juhudi za kutafuta suluhisho la Amani kwa mzozo unaolikumba taifa hilo bado zinaendelea kwa sababu warundi wanataka amani.

Mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika tena Januari 6 mjini Arusha, Tanzania, hayakufanyika kwa sababu serikali ya rais Pierre Nkurinziza ilisema haikuwa tayari kufanya mazungumzo na viongozi fulani wa upinzani ambao iliwaita viongozi wa njama za kuipindua serikali na watu wanaofadhili vitendo vya kigaidi.

Lakini kiongozi huyo wa chama cha FRO-DEBU, Jean Minani amesema juhudi za kutafuta Amani bado ziko hai kwa sababu wa Burundi wanataka Amani. Amesema iwapo serikali ya Nkurunziza haitaki kufanya mazungumzo, italazimishwa kufanya hivyo.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments