Majeshi ya Rwanda(RDF) yavishwa tena medali


Majeshi ya Rwanda yaliyoko kwenye ujumbe wa amani (MINUSCA) nchini Afrika ya kati wamevishwa medali kutokana na utashi, adabu na uzoefu kazini.

Hafla hiyo imefanyika mjini Bangui katika kambi ya kijeshi maarufu kwa jina la Socatel Mpoko Military Camp tarehe tarehe 16 Januari 2016, ikiongozwa na Balozi Diane Corner naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa ambaye pia kwa namna ya pekee anakilisha umoja huo katika jamhuri ya Afrika ya kati.


Balozi Diane Corner akitunuku mwanjeshi wa Rwanda.

Afisa kiongozi anayehusika na masuala ya wafanyakazi kwenye MINUSCA, Lt Col Mensah, amepongeza majeshi ya Rwanda jinsi yalivyoweza kuzuia mashambulizi kwenye Ikulu ya rais ya jamhuri ya Afrika ya kati tarehe 28 Septemba 2015.

Wakati huo waliofanya mgomo walikuwa na mpango wa kushambulia jengo la Rais wa mpito Catherine Samba Panza alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.
Amesema : Mlisimama kidete mkalinda ngazi za uongozi na Ikulu ya rais , wakati huu ngazi zote zinafanya kazi vizuri, asanteni kwa kazi hiyo ya ushujaa’’.

Hafla ya kutunukiwa kwa majeshi ya Rwanda , walikuwepo viongozi mbali mbali wakiwemo waziri katika ikulu ya rais nchini Afrika ya kati, Charles Kenguembat mkuu wa mejeshi ya MINUSCA, Maj Gen Balla Keit ambapo wananchi wamepongeza sana wanajeshi wa Rwanda walioko kwenye ujumbe wa amani Afrika ya kati kwa kazi kubwa wanaofanya.

Christopher Karenzi na
Martin Hubert Ikuramutse

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments