Waziri Mushikiwabo ziarani nchini Israel.


Waziri Mushikiwabo

Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bi Mushikiwabo Louise amefanya ziara ya kikazi nchini Israel.

Tangazo linalopatikana kwa njia ya Twitter ya wizara ya mambo ya nchi za nje, linasema kuwa katika ziara hiyo waziri Mushikiwabo anatarajia kukutana na viongozi tofauti wa taifa hilo ambapo watajadiliana kuhusu ushirikiano wa pande mbili.

Rwanda na Israel ni mataifa ambayo yana ushirikiano mzuri katika sekta mbali mbali.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments