TUJIFUNZE KISWAHILI

Masaa ya kutwa

Yafuatayo ni mafungu ya masaa au nyakati mbali mbali za siku.

WAKATI MAELEZO

Mchana :Ni kati ya adhuhuri na alasiri. Kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni.
Usiku :Kipindi cha siku baada ya kutua jua hadi alfajiri (mapambazuko) .
Alfajiri : Kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi
Macheo Saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi jua linapochomoza
Asubuhi : Mwanzo wa siku jua lichomozapo
Adhuhuri : Saa sita za mchana hadi saa tisa
Alasiri :Saa tisa mchana magharibi
Jioni :Saa kumi na moja hadi saa moja jioni
Machweo/magharibi :saa kumi na mbili hadi saa moja jioni ; jua linapotua
Usikumchanga :Kati ya saa moja jioni na saa sita za usiku
Usikuwamanane :Kipindi cha usiku kutoka saa sita za usiku hadi alfajiri

Martin Hubert Ikuramutse

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments