NAFASI YA USHAIRI KATIKA JAMII YA LEO KWA WANYARWANDA

1

Askofu Alex KAGAME 1912-1981 (Picha/ internet)

Ushairi ni sanaa inayotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia ili kutoa ujumbe.

Shairi ni tungo yenye muundo na lugha ya kisanii inaofuata utaratibu wa vina na mizani, hisia au tukio juu ya maisha au jambo na hufuata utaratibu maalum wa urari na muwala unaozingatia kanuni za utunzi wa mashairi yanayohusika.

Bwana Mloka ni raia kutika nchini Tanzania akiwa ni hodari kwa mashairi anasema kuwa mashairi yameandikwa katika sehemu tatu : Elimu ya jamii, siasa na chemsha bongo katika lugha fasaha.

Katika jamii ya kale ya wanyarwanda, kulikuwepo wanamashairi waiitwao Abasizi ambao walibuni mashairi “Ibisigo” na kuyawasilisha mbele ya mfalme kwa madhumuni ya kumtukuza mfame na ufalme wake.

Miongoni mwao ni kama Nyakayonga ka Musare, Sekarama ka Mpumba na Nyirarumaga hawa ndio wanaojulikana sana.

Sekarama ka Mpumba 1853-1936 (Picha /internet)

Marehemu Askofu Alex Kagame alitunga shairi la kuvutia liitwalo “indyoheshabirayi” hadi leo watu humuheshimu kutokana na usaidizi wake aliyeutoa kwa jamii kwani ni zana, mali, mwavuli na kioo alichotuachia, ni nuru inayotumlikia ili tuone ni wapi tuendapo nasi tusije tukaanguka shimoni.

Katika jamii ya kisasa, mashairi tunayakuta kwenye sherehe za kisiasa, sherehe za wafungao ndoa, vipindi kadhaa vya utamaduni, kwenye vyombo vya habari ama mtu hutunga shairi ili kumsifu mpenzi wake kwa kumuonyesha mapenzi katika maneno matamu. Ibisigo ama imivugo katika lugha ya Kinyarwanda hulinganishwa na mashairi katika kiswahili.

FAIDA YA SHAIRI

Ushairi ni miongoni mwa sanaa muhimu katika jamii ya wanyarwanda hata katika maisha yetu ya kila siku.

Baadhi ya umuhimu wa mashairi ni kama : kukosoa, kukashifu na kubadilisha tabia zisizofaa katika jamii, kukuza Ushujaa, Ujasiri na Uzalendo,kusifia mtu au kitu, kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza,kuhifadhi matukio muhimu ya historia ya jamii, mtunzi na mwasilishi wa shairi anaonyenya hisia zake ama mawazo yake, msanii hukejeli au kukemia mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii, kuibua hisia za kuburudisha na kuhuzunisha,kuelimisha, kuhamasisha na kuzindua jamii.
Kwa jamii ya leo, tunaona kwamba mashairi hayana nafasi kubwa kwani watu yaani vijana hupendelea kujishughulishia katika nyimbo tu bila kutupa jisho kwenye sanaa nyingine kama ushairi.

Hata ndivyo tunashawishi vyombo vya habari kuanzisha vipindi mbalimbali vya burudani vinavyoendeleza sanaa ya ushairi pekee ili jamii ibahatike kuburuwa na mashairi kama kuna vipindi vya burudani vinavyoendeleza na kukuza nyimbo, pia vijana wenye vipaji waanze kutunga mashairi ya kuvutia kwa madhumuni ya kukuza utamaduni na kuelemisha jamii kwa sababu ndio msingi wa nchi na maisha endelevu.

Inafaa Wizara ya michezo na utamaduni iweze kutetea sanaa ya ushairi kwa kuwepo mashindano ya mashairi kila mwaka kuanzia ngazi za mwanzo hadi juu kwa ushirikiano na wizara ya elimu, na taasisi mbali mbali zinazohusika ma masuala ya kukuza lugha ya taifa kama inavyokuwa katika michezo na sanaa nyingine ili kuendeleza, kuelemisha na kukuza utamaduni kupitia mashairi kwa kuhamasisha umoja wa wanyarwanda.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments