DRC yaanza CHAN 2016 kwa kishindo

Congo Kinshasa 3-0 Ethiopia.
Cameroon 1-0 Angola

Timu ya taifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC imeanza mashindano ya 4 kombe la kombe la mataifa barani Afrika CHAN 2016 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ethiopia katika uwanja wa Huye mjini Butare kusini mwa Rwanda.

Mabao hayo yamepachikwa wavuni na Lusadisu , Luvumbu na Munganga

Wachezaji wa Ethiopia wameanza mtanange vizuri huku wakionana lakini ilikuwa kwa muda tu kwani vijana wa DRC wamelisakama lango la Ethiopia sana na katika dakika ya 45, DRC imefunga bao la kwanza kupitia mchezaji Guy Lusadisu.

Wakongomani wakishangilia bao

Kipindi cha pili kimeanza kwa kishindo upande wa DRC, katika dakika ya 46
Luvumbu Hertier anayechezea club ya V.Club , amefunga bao la pili.

DRC imeendeleza mashambaulizi ya hapa na pale kunako dakika ya 56 Nelson Omba Munganga ameandika bao la 3 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Meschack Elia.

Hadi kipenga cha mwisho kupulizwa, timu ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imeondoka na ushindi wa mabao 3-0.

Wachezaji walioanza kwa kila upande

DR Congo : Ley Matampi, Junior Baometu, Joyce Lomalisa, Padou Bompunga, Meschak Elia, Hertier Luvumbu, Nelson Munganga, Merveille Bope,Joel Kimwaki( c) Guy Lusadisu, Jonathan Bolingi Mpangi.

Ethiopia : Abel Mamo, Tesfaye, Anteneh Tesfaye, A. Tamene, T. Dejene, T. Alebechew, Assefa , Panomo, Mamo, T. Tesfaye , R. Lokk

Mechi hiyo, imefuata nyingine ya Kundi B Cameroon na Angola hadi kipenga cha mwisho kupulizwa, Cameroon imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Angola.

Matokeo haya yanaiweka DRC kwenye nafasi ya kwanza na alama 3 na akiba ya mabao 3 ikifuatwa na Cameroon na alama 3 pia ikiwa na akiba ya bao 1.
Nafasi ya tatu ni Angola haina alama haina akiba huku nafasi ya nne ikishikiliwa na ni Ethiopia haina pia pointi na ina deni la mabao 3.

Siku ya tatu ya mashindano ya CHAN, katika kundi C jumatatu tarehe 18 Januari 2015, Tunisia inamenyana na Guinea, saa tisa saa za Afrika ya kati na baadae saa 12 jioni Nigeria itakwaruzana na Niger katika uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments