CHAN 2016 yaanza rasmi, Rwanda inaongoza kundi la A

2

Wachezaji wa timu ya taifa ya Rwanda wakishangilia bao

Jumamosi 16/01/2016

Kundi A : Amahoro stadium

Rwanda1-0 Cote d’Ivoire

Gabon 0 – 0 Maroc

Jumapili 17 Januari 2016

Kundi B : Uwanja wa Huye

15h00 RDC vs Ethiopia

18h00 Cameroon vs Angola

Mashindano ya 4 Kombe la mataifa barani Afrika kwa timu zinazocheza ligi ya nyumbani CHAN kwa kifupi yameanza rasmi jumamosi tarehe 16 Januari 2015 mjini Kigali katika uwanja wa taifa wa Amahoro mjini Kigali.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo, timu ya Rwanda Amavubi imeizaba timu ya Cote d’Ivoire (Elephants) 1-0 lililofungwa na Emery Bayisenge katika dakika ya 15.

Mashindano ya CHAN, yamefunguliwa rasmi na Rais wa jamhuri ya Rwanda Paul Kagame akiwa pamoja na Issa Hayatu Rais wa muda wa Shirikisho la soka duniani FIFA na rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Rais Kagame na Rais wa muda wa FIFA Issa Hayatu

Mechi hiyo ya fungua dimba, imeanza kwa kasi kwa kila upande huku vijana wa Amavubi chini ya mwalimu wa Jonathan Mckinstry wakifanya mashambulizi na katika dakika 15 za mwanzo wamefanikiwa kupata matunda ambapo kijana Iranzi Jean Claude amefanyiwa madhambi karibu na eneo la hatari la Cote d’Ivoire.

Baada ya kufanyika kosa hilo Kijana Emery amefunga bao safi kwa njia ya freeckik, golikipa wa Cote d’Ivoire Ali Sangare amegeuka akakuta nyavu zinacheza.

Wachezaji wa Amavubi stars wakifurahia ushindi

Kipindi cha pili kimeanza huku vijana wa Cote d’Ivoire wakifanya mashambulizi ya hapa na pale lakini ngome ya Rwanda ilikuwa imara.

Kunako dakika ya 58 straika wa Rwanda Jacques Tuyisenge amekokotwa jezi lake na mchezaji Soualia akiwa kwenye eneo la hatari baada ya kona kupigwa. Mwamuzi wa mechi hiyo ameamuru upigwe mkwaju wa penati iliyopewa Bayisenge, golikipa Ali Sangare ameokoa jahazi lake na kutoa mpira nje, baadaye imepigwa kona lakini haikuzaa matunda kwa upande wa Rwanda.

Dakika za mwisho mwisho, Cote d’Ivoire imelisakama lango la Rwanda lakini jinsi muda ulivyokuwa ukiyoyoma ndivyo bahati yao ilivyokosekana. Hadi kipenga cha mwisho kupulizwa, Rwanda imeondoka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya mechi hiyo mtanange wa pili kati ya timu ya taifa ya Morocco na Gabon umeanza hafi kipenga cha mwisho kupulizwa, timu zote zimetoka sare ya kutofungana 0-0.

Gabon na Morocco

Katika kundi A

Rwanda inaongoza na alama 3

Gabon 1

Morocco 1

CIV 0

Wachezaji walioanza
Cote d’Ivoire : Ali Sangare, Marcellin Koffi, Marc Mahan, Essis Bandelaire, Soualio Dabila, Atcho Hemanin,Gbagnon Anicet, Koffi Davy Mahinde, Yace Manius Gregoire, Djedje Frank Guize, Cheick Ibrahim Comara.

Rwanda : Eric Ndayishimiye(Bakame), Ombolenga Fitina, Ndayishimiye Celestin, Rwatubyaye Abdul, Emery Bayisenge, Yannick Mukunzi, Imran Nshimiyimana, , Innocent Habyarimana, Jean Claude Iranzi, Jacques Tuyisenge, Dany Usengimana.

Timu za jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Angola, Cameroon natimu hizi pia zitatumia viwanja vya Amahoro na ule wa Stade Huye.

katika kundi B, Timu ya DR Congo na Ethiopia jumapili tarehe 17 Januari zinatelemka uwanjani kumenyana mjini Huye baada ya mechi hiyo Cameroon na Angola zitamenyana pia.

Makundi ya timu zinazoshiriki mashindano ya CHAN

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments 2

Tumia Comments