CHAN 2016 : CAF yataja Hoteli zilizokubaliwa kupokea timu

Timu zitakazoshiriki katika mashindano ya kombe mataifa barani Afrika kwa timu zinazocheza ligi ya nyumbani ya CHAN, wakati huu CAF imetaja hoteli mpya zitakazopokea timu zote zitakazoshiriki mashindano ya CHAN.

Kundi A mjini Kigali, Gabon itakuwa kwenye Hoteli Umubano Novotel Kacyiru ; Morocco itakuwa Grand Legacy Hotel, wakati Cote d’Ivoire itakuwa kwenye Lemigo Hotel.

Rwanda itakuwa kwenye Golden Tulip La Palisse Nyamata, wilayani Bugesera.
Katika kundi la tatu ,timu zitazokuwa kwenye uwanja wa Nyamirambo , Nigeria itapokewa kwenye Hotel Hill View, Tunisia itakuwa kwenye Hoteli Lemigo, Niger na Guinea zitakuwa kwenye Hoteli Gorilla.

Kundi la pili mjini Huye, timu ya DRC Congo,Cameroon na Ethiopia zote zitapokewa kwenye Hoteli Mater Bon concilli huku Angola ikipokewa kwenye Hoteli Galileo.

Kundi la D mjini Rubavu, Mali iko kwenye Hoteli Serena. Zambia ipo kwenye hoteli Gorilla. Uganda itakuwa kwenye hoteli Belvedere huku Zimbabwe ikipokewa kwenye hoteli ya Western Mountain.

Timu nyingi tayari zimewasili nchini , Uganda inataraji kuwasili jumamosi.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments