BADO KUNA UGOMVI KATI YA UKOMUNISTI NA UBEPARI KWENYE KARNE YA LEO ?

Nyundo na Mundu, ni alama ya ukomunisti, nguvu ya wafanyakazi.

Ukomunisti ni mfumo wa kiuchumi, kijamii na kisiasa usemao kuwa watu wa kila sehemu ya dunia wanapaswa kumiliki zana, viwanda, na mashamba, ambayo yanatumiwa kuzalishia bidhaa na vyakula. Mchakato huu wa kijamii hujulikana kama umiliki wa kawaida. Katika jumuia ya wakomunisti, hakuna mali binafsi, pia itikadi ya chama cha siasa kinachofuata mfumo huu.

Ubepari ama ubeberu ni mfumo wa kiuchumi unaowezesha watu wachache kumiliki raslimali na njia kuu za uchumi wa nchi. Kati ya sifa za ubepari kuna ulimbikizaji wa mtaji, ushindani katika soko huria na kazi zinazilipwa mshahara.

Katika karne ya 20 kulitokea ugomvi wa ukomunisti na ubepari, na hivyo tunaviona kwenye vita baridi ambavyo vimekuwepo miaka 38. Chanzo kilikuwa farakano kati ya washindi wa Vita vikuu vya Pili ya Dunia.

Hapo ndipo dunia nzima imeona nguvu za mifumo hiyo lakini kwa dunia ya leo ingawa kunabaki misuguano kati ya pande hizo mbili za mikumi.

Marekani, Umoja wa Kisovyeti, Uingereza na Ufaransa zilikuwa nchi washindi wa vita hii dhidi ya Ujerumani. Urusi ulikuwa na siasa ya kikomunisti lakini washindi wengine walifuata siasa ya kidemokrasia pamoja na uchumi wa kibepari.

Pande zote mbili zilijenga jeshi kubwa na kuwa na silaha nyingi lakini hazikuanzisha vita moja kwa moja ingawa zilijaribu kutishana na kupeana matatizo kwa njia nyingi.

Kipindi hiki kilikuwa na maandilizi ya vita lakini vita ya kijeshi haikuanza. Sababu muhimu ya kutoingia katika mapigano ya wazi ilikuwa akiba kubwa ya silaha za nyuklia kila upande na wote walijua ya kwamba vita ingeleta uharibifu kabisa kwa nchi zote zilizoshiriki hata kwa dunia yote.

Nchi za Magharibi ziliunda muungano wa kijeshi wa NATO (North Atlantic Treaty Organization) wakiahidi kushikamana kama nchi yoyote ingeshambuliwa na nje.

Wasovieti walijibu kwa kuunganisha nchi zilizokuwa chini ya usimamizi wao katika Mapatano ya Warshawa. Miungano haya ya kijeshi yalifuatwa na mapatano ya kiuchumi kila upande.

Ukuta wa BERLIN ulijengwa ili kutenganisha Ulaya mashariki (ukomunisti) na ulaya magharibi (ubepari) lakini Anguko la ukuita wa Berlin ilikuwa dalili ya mwisho wa vita baridi na pia utawala wa kikomunisti katika nchi za Ulaya.

Ilionekana kwamba upande wa Marekani ulishinda upande wa umoja wa Kisovieti kwa sababu uchumi wa ubepari ulikuwa umeishaendelea na Umoja wa Kisovyeti ullitia nguvu jeshi na maendeleo ya silaha lakini uwezo wa kiuchumi haukutosha.

Na viongozi kwa pande zote wakatia sahihi ya kusimamisha vita baridi mnamo 1989.

Katika nchi ya Tanzania Rais wa zamani wa nchi hiyo Hayati Mwalimu Julius Nyerere (Baba wa Taifa) alianzisha mfumo uitwao ”Ujamaa” yaani ulikuwa na malengo ya kuwepo kwa chama kimoja Chama Chama Mapinduzi (CCM), kukomesha ubaguzi kwa misingi ya hali ya mtu, kupeleka uzalishaji katika vijiji, kujitegemea kwa nchi bila kungoja fimbo ya ambali ambayo haimuiwi nyoka na elimu kwa watanzania wote bila malipo.

Punde si punde wananchi walianza kuvuna matunda kidogo lakini Ujamaa ulishindwa kwa sababu ya kuporomoka kwa bei ya bidhaa zilizozalishwa nchini humo, vita vya Uganda na Tanzania, na ukame wa miaka miwili kwa mfululizo.

Nchini kote Tanzania uchumi uliyumba, sekta ya viwanda ilididimia, barabara zikaharibika sana, Serekali hatimaye ilitoa ahadi ambazo ziligeuka kuwa uongo.

Hayo ykiarifiwa , Che Guevara alitumwa na Cuba baada ya kifo cha Patrice Emery Lumumba aliyewahi kuwa waziri mukuu wa Zaire ili kumtetea Laurent Desire Kabila wa DRC kwa shabaha kuu ya kumuondoa madarakani Mobutu Seseseko baada ya kutangaza kuwa anakubali mfumo wa ubepari lakini alishindwa vita hiyo kwa sababu ya kutoelewana na Kabila baada ya kutoelewana kitabia kwani Kabira alionekana vitani mara moja na wenzake walikuwa wakifanya biashara zao pia na mara nyingi wapiganaji walikuwa wakivuta bangi.

Leo kuna nchi zinazofuata mfumo wa Kikomunisti ambazo ni :
China, Korea kusini, Vietnam na Cuba. Hizi ndizo nchi zijulikanazo rasmi kuwa ni nchi za kikomunisti duniani, marais wengi huogopa kufuata mfumo huo lakini watu wengi hudhani kuwa ukomunisti ni mfumo mzuri kwa sababu hakuna mali ya mtu binafsi yaani huchukua atakacho kwenye jamii yake lakini ukitazama pande zote mbili kuna ubora na udhaifu.

Kiukweli, leo hakuna upinzani mkubwa kati ya ukomunisti na ubepari kama ilivyo kuwa awali kwani tunaona kuwa ukomunisti hauna nguvu bali hubaki historia tu.

IKURAMUTSE Martin Hubert

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments