Polisi yaahindi kuwa usalama wa mashabiki wa CHAN utakuwa shwari

Msemaji wa Jeshi la polisi nchini Rwanda, ACP Celestin Twahirwa

Polisi ya Rwanda imetangaza kuwa iko tayari kulinda usalama wa mashibiki na watu wote watakaohudhuria michezo ya kombe la kimataifa la CHAN.

Akipitisha kwenye mtandao wa Twitter wa Polisi nchini , msemaji wa polisi mheshimiwa ACP Twahirwa Celestin amesema kuwa mwisho wa mechi timu iliyoshinda washabiki hufurahia kwa shangwe kiyasi kwamba inaweza ikasababisha ajali.

ACP Twahirwa amesisitiza kuwa polisi iko tayari na makini kulinda usalama wa raia.

Polisi imeahidi kuwa maeneo ya viwanja vitakavyotumiwa kwa michezo kutakuwa na ulinzi wa hali ya juu.

Mashindano ya Kombe la kimataifa la CHAN yataanza siku ya Jumamosi tarehe 16 Januari 2016, na kumalizika hapo tarehe 7 Februari 2016.

Bagabo John

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments