ONDOA MADHAI YA KUWA KISWAHILI NI KIARABU...

1

Profesa Malcon Guthrie}

ONDOA MADHAI YA KUWA KISWAHILI NI KIARABU

Kiswahili ni lugha ya kiafrika inayojulikana hasa hasa kwenye nchi za Afrika ya Mashariki.

Si mara ya kwanza tumewahi kusikia habari zinazoenea kwenye masikio yetu husema kuwa Kiswahili ni lugha iliyozaliwa na kiarabu, hivi tunavikuta kwenye maongezi na masimulizi ya umati wa watu hata na wengine husema kwamba Kiswahili ni lugha yenye asili ya kiafrika.

Tungependa kuwaelezea kwamba Kiswahili ni lugha yenye asili ya kiafrika na ni lugha ya kibantu. Kiukweli hakuna lugha isemwayo kuwa inajitosha kwenye misamiati yake ya asili ni lazima ikope misamiati kadhaa kwenye lugha nyingine. Lugha inakua kama tecknohama inavyoendelea, pia lugha inakufa kutokana na sababu mbalimbali.

Kiswahili kilianza kuandikwa kwa herufi za kiarabu pekee kwa karne nyingi. Wafanyabiashara kutoka uarabuni, ujerumani na uhindi walikuja huko pwani ya afrika na lugha kuu ya biashara ilikuwa kiarabu.

Sababu nyingine watu wanavyosema kuwa Kiswahili ni kirabu ni asili ya neno Kiswahili yaani “Sahil”. Kwa kiarabu ina maana ya ukanda wa ardhi iliyolimwa yenye miji au vijiji vilivyo kando kando ya bahari. Waarabu walimwita mtu wa pwani kwa jina la “Sahila” jina lilirekebishwa na kufuata muundo wa lugha za kibantu, jina la watu waliokuwa wakiishii pwani likawa waswahili na lugha yao ikawa Kiswahili na utamaduni na utu wao ni uswahili.

Inadaiwa kwamba maneno yenye asili ya kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya kiarabu baadhi ya maneno hayo ni kama : bin adam, takriban n.k.
Pia inadaiwa kwamba Kiswahili kilianza pwani, idadi kubwa sana ya wenyeji wa pwani ni waislamu, na kwa kuwa uislamu uliletwa na waarabu basi Kiswahili nacho kililetwa na waarabu

Kiswahili si kiarabu kutokana na sababu zifuatazo :

Matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.

Katika lugha zote za kibantu, maneno huishia kwa irabu, wakati ambapo maneno katika kiarabu huishia na konsonanti.

Kiarabu Kiswahili
Surat Sura
Ayat Aya
salah sala

Majina ya Kiswahili hupangika katika ngeli, umoja na wingi
Kiswahili kina miundo ya maneno kama lugha za kibantu
Maneno lugha
Nakwenda Kiswahili
Nagenda Kihaya
Natonga Kipare
ndagenda kinyarwanda

Kiswahili kina muundo wa maneno mawili kama : mwanahewa, pundamilia, mitishamba n.k.
Kiswahili kina maneno yenye uwezekano wa kunyumbulika na kunyambulika kama lugha zingine za kibantu
Kiswahili : kucheka, kuchekesha, kuchekelea, kuchekana
Kindali : kuseka, kusekasha,kusekelela.
Kibena : kuheka, kuhekesha, kuhekelea

Kiukweli hawa wanavyosema kwamba Kiswahili ni kiarabu kutokana na jina lenyewe la Kiswahili, hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalau hajiiti jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine : jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya afrika mashariki.

Kwa kigezo cha dini nacho hakikubaliki, lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya kiarabu ilikuwepo karne nyingi kabla ya kunuliwa dini ya uislamu na lugha za kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla kununuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kiingereza au kijerumani si ukristo, basi ndivyo hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya uislamu, aslant ! Wala kiarabu nacho si uislamu.

Utofauti wa kusema kwamba Kiswahili hakikuwepo kabla ya kufika kwa waarabu unatokana kwamba hakuwepo na maandishi , ikumbukwe kuwa kutokuwepo nyaraka haina maana kwamba lugha haikuwepo. Kufanya hivyo ni kuchukuwa uamuzi wa juu juu.

Kutayarisha habari hii tumetumia maandishi ya wataalam kwenye isimu kama Profesa C. Maganga, Profesa Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dakt. C. Rohl.

IKURAMUTSE Martin Hubert.

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments