CHAN : Waafrika wote wanaotaka kuhudhuria mechi hakuna malipo ya visa

Waziri Uwacu Julienne akiwa katikati

Rwanda imesema imejiandaa vya kutosha kwa mashindano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani, maarufu kama CHAN.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari waziri wa michezo Uwacu Julienne amesema kwamba serikali imeondoa malipo ya visa kwa Waafrika wote watakaotaka kuhudhuria mechi za CHAN.

Waziri Mushikiwabo

Amesema : "Kila kitu kiko tayari …viwanja, mahoteli, usalama na mahitaji yote ya kuandaa mashindano ya kiwango hiki."

Ameongeza kuwa miundombinu pekee yaani ujenzi na ukarabati wa viwanja vitakavyotumiwa, iliigharimu serikali milioni 18 dola za Marekani.

Mashindano ya CHAN yataanza kutimua vumbi tarehe 16 mwezi huu.
Mechi ya ufunguzi ni kati ya wenyeji Rwanda na Ivory Coast kwenye uwanja wa taifa Amahoro.

Viwanja vingine vitakavyotumiwa ni uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, uwanja wa Huye Kusini mwa nchi na uwanja wa Umuganda mjini Rubavu karibu na mpaka wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Timu ya taifa ya Rwanda ilicheza mechi mbili za kirafiki na Cameroon na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kabla ya mashindano ya CHAN kuanza rasmi. mchuano wa kuanza ilienda sare ya kufungana na Cameroon 1-1 na mchuano wa pili iliwazaba DRC 1-0 katika uwanja wa Umuganda.

Makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments