Wizara ya michezo na Utamaduni itaongeza viwanja vya ukumbi

Waziri Uwacu Julienne

Waziri wa michezo na utamaduni bi Uwacu Julienne amesema kuwa mwaka huu majengo ya ukumbi yataongezeka pia na wajasiliamali kuwekeza katika mradi huo.

Zimepita siku ikisadikiwa kuwa kuna uhaba wa viwanja vya ukumbi au majengo ya burudani.

Kwa mjibu wa gazeti la Kigali today hili lilikuwa swali ambalo alikuwa akiulizwa waziri wa michezo na utamaduni katika miaka ya hapo awali.

Waziri Uwacu amesema kuwa mwaka huu angalau utakuja kufika ukingoni kukiwa na majengo yaliojengwa kwaajili ya michezo.

Pia waziri ameongeza kusema kuwa mwaka wa bajeti 2016-2017 kutakuwa na pesa zitakazokuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanja hivyo.

Wakati bado wakiwa katika mradi huo wakujenga viwanja vya ukumbi, waziri amesema kuwa watakao aka kuaanda tafriji tofauti hususani wasanii wanaweza kutumia viwanja vya serikari vilivyoko maeneo tofauti nchini.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments