Marais wa EAC kuzungumzia suala la Burundi na Rwanda

Marais wa nchi za muungano wa Afrika mashariki EAC. wanatarajiwa kuongelea kuhusu suala la Burundi na Rwanda.

Marais wa EAC wanatarajiwa kuzungunzia swara la mashitaka ya serikali ya Burundi inaposhutumu Rwanda katika mzozo unaoendelea nchini Burundi.

Wazili wa jeshi nchini Uganda ambae pia ndie mpatanishi katika mazungumzo ya kurejesha amani nchini Burundi bwana Crispus Kiyonga ameviambia vyombo vya habari ya kuwa hivi karibuni kutafanyika mkutano iri kuingilia kwa kina mashtaka Rwanda inayoyakana kuhusika na mzozo wa Burundi.

Kiyonga amesema kuwa miongoni mwa shutuma zinazotolewa na Burundi ni pamoja na kuwapereka jeshini vijana wa kirundi walioko katika baadhi ya kambi zilizowapokea kama wa kimbizi nchini Rwanda, shutuma hizo ziritupiliwa mbali na serikali ya Rwanda ikisema kuwa huo ni uongo mtupu.

Mzozo huo nchini Burundi ulizuka mara tuu Rais Nkurunziza aliposema kuwa atagombea tena kuwa Rais katika awamu ya tatu, ambapo wapinzani wake pia na walisema kuwa ni kinyume na katiba ya nchi.

Tangu kuanza kwa machafuko nchini humo wakimbizi wapatao elfu 73 wako katika kambi tofauti nchini Rwanda.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments