Rwanda yaziondolea nchi 15 zitakazoshiriki kombe la CHAN pesa za kutafuta Visa

Akiongea kupitia Radio ya Taifa kuhusu maandalizi ya michuano ya kombe la CHAN ilipofikia. waziri wa michezo na utamaduni bi Uwacu Julienne, amesema kuwa kuondoa pesa za kutafuta visa itawarahisishia watakaoshiriki katika kombe hilo kuja kwa wingi kushabekia timu zao.}]

Uamuzi huo wa kuondoa pesa hizo umechukuliwa ili kuwarahisishia wale wote watakaotaka kuja kutembelea Rwanda.

Pesa zipatazo bilioni 16 na milioni 200 ndizo zilizotengwa kwa bajeti ya kombe la CHAN 2016.

Kuhusiana na usalama katika viwanja vya mpira, msemaji wa Polisi nchini ACP Twahirwa Celestin amesema kuwa kuhusiana na viwanja vitakavyotimiwa kwa mechi vimekwishafanyiwa ukaguzi wa kiusalama, kwa hiyo jeshi la polisi liko makini katika kulinda usarama.

Tuwakumbushe kuwa kombe hilo la CHAN litaanza hapo rasmi tarehe 16 Januari hadi tarehe 7 Februari 2016.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments