Balozi Hope Tumukunde tayali amekubariwa kusimamia Rwanda nchini Ethiopia

Balozi wa Rwanda nchini Ethiopia bi Hope Tumukunde tayari amekwishafikisha nyaraka za kusimamia Rwanda nchini Ethiopia

Nyaraka hizo amezifikisha kwa naibu katika wizara y ya ushirikiano na nchi za nje nchini Ethiopia bwana Taye A Selassie.

Baada ya kukabizi nyaraka hizo, balozi bi Tumukunde Hope amesema kuwa atafanya juu na chini ili ushirikiano kati ya Rwanda na Ethiopia uzidi kuimarika.

Katika upande wa Ethiopia bwana Taye A Selassie amesema kuwa ana matumaini kwamba ushirikianao wa nchi hizi mbili utazidi kudumishwa.

Bi Tumukunde aliteuliwa kusimamia Rwanda nchini Ethiopia kupitia mkutano wa baraza la mawazrli uliofanyika hapo tarehe 9 Septemba 2015, alipochukuwa nafasi ya Mitali Protais ambaye alikuwa ametoweka nchini kwa shutuma za wizi wa pesa milioni zipatazo 50 za Rwanda kupitia chama chake cha PL.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments