Muungano wa Afrika mashariki kuanza kutumia Pasipoti moja hivi karibuni

Richard Sezibera

Jumuiya ya Afrika ya mashariki (EAC) umetangaza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu itaanza kutowa pasipiti moja itakayotumiwa na nchi tano zinazojenga jumuiya hiyo.

Tangazo ambalo limetorewa na katibu mkuu wa EAC mheshiwa Dr. Richard Sezibera, amesema kuwa pasipoti hizo zitawarahisishia safari wakazi wa Rwanda, Uganda,Kenya,Tanzania pia na Burundi.

Pia Dr. Sezibera ameongeza kuwa pasipoti hizo nimojawapo ya njia ya mafanikio katika inchi za EAC.

" Ninajivunia kuwa EAC imepiga hatuwa ya kimshikamano katika maendeleo ya nchi hizo." Alisema

Kwa kawaida, Pasipoti nchini Rwanda ilikuwa ikitolewa kwa gharama ya faranga elfu hamsini za Rwanda .

Pindi shughuli hizo za maandalizi zitakapokuwa zimemalizika, inatarajiwa kuwa mwaka kesho 2017 wanaotaka pasipoti kwenda kati ya nchi mojawapo za muungano wa Afrika mashariki wataanza kutumia pasipoti hizo.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments