Waziri Mushikiwabo amewakaribisha watakaoitikia mashindano ya CHAN 2016.

Waziri Mushikiwabo

Kupitia kwenye Twitter, Louise Mushikiwabo, waziri wa Rwanda anayeshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa ambae pia ni msemaji waselikali amewapa karibuni wachezaji wa timu za Afrika waliokuja katika michuano ya kombe la kimataifa CHAN 2016 pia na mashabiki watimu zao.

Bi Mushikiwabo amesema kuwa Rwanda inawapa karibuni wachezaji pia na mashabiki wo, kujisikia kama nyumbani.

Michuano ambayo inatarajia kuanza hapo rasmi tarehe 16 Januari 2016 na kumalizika tarehe 7 Februari. 2016.

Mechi hizo zitafanyika katika viwanja tofauti vikiwemo kiwanja cha Amahoro Stadium, uwanja wa Kigali. uwanja Huye, na Uwanja wa Rubavu.

Timu zitakazoahiriki katika michuano hiyo nipamoja na Rwanda ambayo ndie mwenyeji, ni pamoja na Uganda,Ethiopia, Maroc, Tunisia, Mali, Guinea Niger, Cote d’Ivoire, Nigeria, Cameroon, Gabon, RDC, Zambia, Angola pia na Zimbabwe

Timu hizi zote zimegawanyika katika makundi ambayo ni A,B,C,D.

Mchezo wa kirafiki uliochezwa Jana kati ya timu ya Amavubi ya Rwanda na timu ya Cameroun, walitoka sale wa kifungana bao 1-1.

Mechi ya kufunguwa michuano itazikutanisha timu ya Amavubi ya Rwanda pia na timu ya Cote d’ivoire katika uwanja wa Amahoro stadium hapo tarehe 16 Januari saa kumi na mbili jioni saa za Afrika ya mashariki.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments