Wabunge waiomba serikali kuvalia njuga wavulana wanaokana waliopachika mimba

Wabunge pia wanaohusika na faida za wanawake wameiomba serikali kuchukuwa mikakati vijana wanao wabebesha mimba wasichana na baadae kukana kwasadiia kulea wanao.

Swala hili limewasilishwa bungeni na baadhi ya ya wabunge wenye majukumu ya ustawi wa jamii na uchumi (RPRPD) kwa kifupi

Kwa mujibu wa Gazeti Igihe.com linavyoalifu ni kwamba mbunge Hon John Luku Rwabyoma amesema kuwa swala ra vijana na baadhi ya wa kina baba linapaswa kupewa kipaumbele kama inawezekana kwa makosa wanayoyafanya wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Amenukuliwa : " Ni kwa nini tunasikia binti amebebeshwa mimba na mvulana lakini usumbufu wote unakuta uko kwenye binti na wakati kijana yuko katika hali ya kawaida"

Naibu katika wizara ya familia Bi Henriette siku zilizo pita alisema kuwa vijana ambao watakuwa wanakana watoto wao baada ya kufanya mapenzi na binti siku zao ziko ukingoni

Hivi punde Rwanda itaanzisha jinsi ambavyo watakuwa wanapima damu maarufu (DNA/ADN) ili kudhibitisha kuwa mtoto niwa huyo mvulana aliyembebesha binti huyo mimba, ili swala la kuwakana watoto liweze kupatiwa suluhu.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments