Kamishina wa tume ya taifa amelaani jeshi la DRC

Sayinzoga Jean

Kamishina wa tume ya taifa inayo husika na kuwalejesha waliokuwa askari katika maisha ya kiraia Mheshimiwa SAYINZOGA Jean ameliambia gazeti la Kigali Today kuwa jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa kuwa halikuweza kufanikiwa kuwapokonya silaha waasi wakundi la FDLR walioko katika misitu ya DRC.

Sayinzoga amesema kwamba jeshi la DRC lilipuuzia kwa makusudi kuwa pokonya silaha kundi la FDLR kwani wangekuwa wan taka kuwa pokonya silaha, wangefanya kama walivyo weza kufanikiwa kuwapokonya waasi wa kundi la M23 walivyo fanya wakishilikiana na Monusco.

Amesema : "je kama walikabiliana na FDLR walifanikiwa kuwakamata waasi wangapi ? waliwauwa wangapi ? shuguli za kukabiliana na FDLR sisi tunaona hazikuzaa matunda yoyote. Kama wangelifanya kwa juhudi basii waasi hao wangekuwa tayari. wangeisha weka siraha chini nakurejea nchini."

Ripoti iliyotorewa na Umoja wa mataifa UN ilionyesha kuwa shughuli za kupambana na FDLR kuwapokonya silaha hazikuzaa matunda.

Kamishina SAYINZOGA, ametaja takwimu za wale tayali waliojisalimisha na kuweka chini silaha.

Mwaka 2010 walirejea waasi wa FDLR wapatao 549, mwaka 2011, wapatao 963, mwaka 2012, 1800, mwaka 2013, 524.

Kulingana na takwimu hizo Sayizonga amesema kuwa hazilizishi. Kutokana na majukumu waliyo kuwa nayo ya kuwapokonya silaha waasi wa kundi la FDLR walioko katika misitu ya DRC.

Bagabo John

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments