Rais Kagame ziarani katika Mataifa ya muungano wa kiarabu

Rais Kagame na viongozi wa Muungano wa mataifa ya kiarabu mwaka jana/Photo Izuba Rirashe

Rais wa jamhuri ya Rwanda Paul Kagame yuko ziarani katika Mataifa ya muungano wa kiarabu ambapo amezungumza na mwanamfalme wa huko Sheikh Mohamed Bin Zayed Al Nahyan.

Gezeti la Gulftoday limetangaza kuwa viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu uchumi na uwekezaji na matataizo mengine yanayoikabili dunia na namna ya kuyatatua.

Mwaka jana, rais Kagame alifanyia ziara nyingine huko wakati alipohudhuria mukutano wa kuchunguza namna za kuwekeza barani Afrika na kuvutia wawekezaji kuwekeza barani humo pamoja na kukuza miundombinu.

Mataifa ya muungano wa kiarabu ni nchi tajiri kwenye mafuta, na inanyakuwa nafasi ya tisa duniani kwa kuuza mafuta mengi duniani.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments