Keza Joanna atawazwa kuwa balozi wa utamaduni duniani ‘Miss Heritage Culture Ambassador’

Mrembo wa utamaduni 2015,nchini Rwanda Keza Bagwire Joannah jumatatu wiki hii tarehe 04/01/2016 alikabidhiwa cheti cha kuwa balozi wa utamaduni duniani kati ya wasichana 80 waliokuwa kwenye mchakato wa kutafuta taji la urembo wa utamaduni duniani ‘Miss Heritage World 2015’ uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.

Keza Joannah -Miss-Heritage-Word-2015 mwakilishi wa Rwanda sasa ni balozi wa utamaduni duniani

Nchini Afrika ya kusini Tarehe 15 Novemba 2015 kulifanyika uchaguzi na kutoa taji kwa mrembo wa utamaduni duniani ambapo Ziphozinhle Ntlanganiso ndiye aliyevishwa taji hilo.
Kulingana na gazeti la Umuseke, Ishimwe Kagame Dieudonne kiongozi wa Rwanda Inspiration Back Up inayoandaa Miss Rwanda, amesema kuwa habari kuhusu kutunukiwa Miss-Heritage-Word-2015 ni za ukweli.Walizipokea mwanzoni mwa mwaka huu.
Amesema : Tangazo hilo tumelipokea kutoka kwa waandalizi wa shindano hilo duniani jumatatatu asubuhi, ameongeza kuwa ni furaha kwa Keza Joannah pamoja na wanyarwanda kwa jumla’’.

Ameongeza kuwa bila shaka Rwanda inakwenda taratibu ikibadili sura yake ulimwenguni

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments