Rais Kagame ajibu marekani kuwa Rwanda haitothubutu kuwa mzigo wao

Rais Kagame/photo.net

Rais Paul Kagame amejibu Marekani kuwa haitakiwa kuhuzunishwa na matatizo ya wanyarwanda bali wanyarwanda wenyewe ndio watakaobeba mizigo na matatizo yao.

Rais Kagame amejibu wamerekani siku moja baada ya kutoa tangazo likisema kuwa wamehuzunishwa na hotuba ya rais Kagame wakati wa mkesha wa mwaka mpya 2016, ambapo aliwakubalia wanyarwanda kuwa ataongoza taifa baada ya mwaka 2017 kama alivyokuwa amewaahidi.

Kupitia Twitter, Rais Kagame, Jumatatu ya tarehe 4 Januari 2016 amesema kwamba yaliyofanywa na wanyarwanda hayakulenga kuwaumiza wamarekani na hawana mpango unaolenga kuwaumiza wamarekani.

Rais Kagame ameendelea kusema kuwa barani Afrika kuna mengi ya kuhuzunisha kuliko kuhuzunishwa na uchaguzi wa wanyarwanda.

Amesema : ‘’Masuala ya Afrika ni kama umasikini, maradhi , uongozi, teknolojia hayo yote hayawezi kupewa majibu ya kile kilichojificha baada ya kuhuzunishwa’’.
Marekani, Uingereza na jumuiya ya Umoja wa Ulaya zimesema zinahitaji kukabidhiana madaraka nchini Rwanda itakapofika mwaka 2017.

Rais Kagame alisema kwamba wakati ukiwadia nchini Rwanda kutafanyika mapokezano kwa nia ya amani.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments