Tour du Rwanda 2016 : Kwa mara ya kwanza Rusizi watashuhudia mbio za baiskeli

Bingwa wa Tour du Rwanda JB Nsengimana ataraji kuelekea kwenye timu ya Bike Aid ya Ujerumani

Timu ya taifa ya Rwanda imeeanzaa maandalizi ya kusaka ubingwa wa Tour du Rwanda mwaka 2016 wakianzia nchini Gabon kabla ya kuelekea kwenye mashindano ya Afrika (African Championships) yatakayofanyika mwezi ujao februari tarehe 21-26 nchini Morocco pamoja na kuzunguka Algeria mwezi machi.

Janvier Hadi mwenye umri wa miaka 24, ambaye alikata tikiti ya kushiriki mashindano ya Olimpiki nchini Brazil mwaka huu ataongoza timu ya taifa ya Rwanda itakayoshiriki mashindano ya kuendesha baiskeli ya La Tropicale Amissa Bongo nchini Gabon kuanzia Januari 18-24.

Kwa mujibu wa The New times, mwenyekiti wa chama cha kuendesha baiskeli nchini Rwanda FERWACY) Aimable Bayingana, mashindano haya ya kimataifa
yatakayofanyika kwa mara ya nane, yatakuwa na changamoto kubwa kwa timu ya taifa kwa sababu wachezaji wawili mashuhuri Nsengimana na Janvier Hadi watakuwa wakichezea timu ya Bike Aid ya Ujerumani.
Ameongeza kuwa inabidi sasa kuandaa wengine, ambao wana vipaji vya kuendesha baiskeli.

Amesema : ‘’Ninaamini kwamba wachezaji watu watafanya vizuri bila kujali walioondoka’’.
Bingwa wa Tour du Rwanda JB Nsengimana ataraji kuelekea kwenye timu ya Bike Aid ya Ujerumani

Aidha, Bayingana ameongeza kuwa mashindano ya Tour du Rwanda mwaka huu wa 2016 yamepanua safari hadi wilayani Rusizi kiasi kwamba mashabiki na wapenzi wa mbio za baiskeli katika eneo la magharibi ya nchi, watanufaika kujionea mashindano ya kimataifa waliyokuwa wakisubiri kwa hamu

Mwaka uliopita 2015, Hadi alinyakua nafasi ya 9 barani Afrika katika mashindano ya (road racing), ushindi huo ulimuwezesha kukata tikiti ya Rio de Janeiro, Brazil kuanzia tarehe 6 hadi 21 Agosti 2016.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments