Watu wapatao laki moja waliohukumiwa na Gacaca wamaliza kifungo jela

Mahabusu waliomaliza hukumu yao kutokana na mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi 1994, wanaishi vyema na manusura wa mauaji ya kimbari.

Kulingana na Umuseke.com, katika wilaya mbali mbali nchini Rwanda kunalipotiwa takribani watu laki moja (100,000) waliokwisha maliza kutumikia kifungo chao jela baada ya kuhukumiwa na mahakama za kijadi maarufu "GACACA" kwa kuhusika na mauaji ya kimbari dhidi ya watusi mwaka 1994 nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Kamishina Jean Baptiste Kambanda, mkuu wa idara ya afya na ustawi wa jamii katika mahabusu nchini Rwanda, alidsema kwamba katika kitengo cha mahabusu tangu kuachiliwa huru kwa wale waliokwisha maliza kifungo chao jela walioachiliwa huru hivi sasa wanaishi vyema na manusura wa mauaji ya kimbari baada ya kuwaomba msamaha na kukili walioyoyatende na kubaini kuwa hayastahili jamii.

Takwimu zilizotolewa na Kamishna Kambanda zinaonyesha kuwa kwa muda wa miaka miwili ijayo hadi mwaka 2017, watu wapatao 3,220 watakaokuwa wamemaliza hukumu yao wataachiliwa huru huru na kurudi makwao pia inatarajiwa ifikapo mwaka 2018- 2020 wataachiliwa huru wengine wapatao 2,600.

Katika ushuhuda uliotolewa na Bwana Musabyimana Emmanuel mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa kitongoji cha Kamuvumyi ambaye alikuwa amehukumiwa miaka 8 kutokana na kuhusika kwake kwenye mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi

Mara baada ya kumaliza kifungo chake jela, alisema kuwa baada ya kurudi nyumabani kwake alipokelewa vyema na wale aliowakuta pia ameongeza kuwa hata aliyemshitaki kuhusika na mauaji hayo hivi sasa ndiye jirani mwema licha ya bwana huyo Emmanueli kusema hivyo, na mwenzake Musabyimana Albert mwenye umri wa miaka 50 baada ya kutumikia kifungo jela kwa kipindi cha miaka 19 na kuachiliwa huru. Alipomaliza kifungo chake naye pia amesema kuwa anaishi vizuri na majirani zake.

Wakati huu katika magereza tofauti nchini wamesalia mahabusu wapatao elfu 35 waliohusika na mauaji ya kimbari, tayari wameisha hukumiwa kifungo jela kwa kosa la mauaji ya kimbari dhidi ya watusi mwaka 1994.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments