Kocha wa Vital’o Kanyankore asimamishwa kazi ya ukufunzi


Chini ya uongozi wa Kocha wa Vital’o Gilbert Kanyenkore maarufu kwa jina la Yaoundé, ameachishwa kazi tarehe 31 Disemba 2015 na nafasi yake imenyakuliwa na Etienne Ndayiragije, kocha wa zamani wa LLB Sport4 Africa.

Kwa mujibu wa gazeti la Iwacu nchini Burundi, kwa muda wa miaka 26 timu hiyo ya Vital’o ilikuwa chini ya uongozi wake Kocha Kanyankore, ambapo imetwaa vikombe vingi na wakati huu ilikuwa ikijiandaa mashindano ya kombe la mabingwa barani Afrika (Ligue des Champions Africaine 2016). Timu hiyo itachuana na Lioli FC ya Lesotho tarehe 14 Februari 2016.

Mashabiki na wapenzi wa timu hii wameshangazwa na hatua hii ya kumuondoa ki ghafla kocha Kanyankore ambaye aliwahi kuwa mkufunzi msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda B iliyotwaa kwa mara ya kwanza kombe la Afrika ya kati na mashariki CECAFA challenge nchini Rwanda, aliwahi pia kuwa mkufunzi wa timu ya Les Citadins ya jiji la Kigali na Rayon sport.

Gilbert Kanyenkore Yaoundé, ni kocha anayeheshimiwa sana nchini Burundi hajafahamishwa sababu ya kuondolewa katika timu yake.

Mwaka 1992 Vital’o ilicheza fainali ya kombe la Afrika chini ya uenyekiti wa Mzee Grégoire Muramira.

Habari ambazo tumepokea hivi punde ni kwamba Kocha Kanyankore ameteuliwa kuwa
mshauri na atakuwa akijihusisha na masuala ya scouting katika club ya vital’o. Kocha msaidizi wa timu hoyo alikuwa amefutwa kazi lakini amerudishwa ndani ya club hiyo

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments