Au yashinikiza Burundi ikubali kupokea jeshi la kulinda amani

Dlamini-zuma

Umoja wa Afrika AU, umesema kwamba unaweza ukachukulia hatua pande zote husika katika machafuko yanayoendelea nchini Burundi.

AU imelitaka taifa la Burundi kukubali jeshi la umoja wa mataifa kuingia nchini na kuweza kuzuia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Kulingana na Igihe.com, AU iliomba taifa hilo kukubali kupelekwa kwa wanajeshi wapatao 5000 wa kulinda amani nchini humo ambapo jeshi hilo lilikuwa limepewa jina la "Mission Africaine Pour la Prevention et la Protection au Burundi kwa kifupi " MAPROBU".

Hayo yakiarifiwa, Bi Zuma amewatolea wito viongozi wa makundi yanayozozana kuhudhuria kwenye meza ya mazungunzo kuhusu mzozo nchini Burundi, mazungumzo yanayo tarajiwa kufanyika mwezi January 2016 Arusha, Tanzania.

Dlamini-zuma amesema kuwa AU iko tayari kutoa msada ikiwa Burundi itakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo ya kupereka jeshi hilo.

Dramini-zuma ameongeza kuwa kupeleka jeshi la kulinda amani, italeta matumaini kwa wananchi wa taifa hilo.

Wakati Raisi Nkurunziza alipotangaza kuwania uraisi katika awamu ya tatu wanainchi walisema kuwa ni ukiukwaji wa katiba ya nchi, kwani katiba ya Burundi inasema kuwa Rais anapaswa kuwa madarakani kwa kipindi cha mihula miwili pekee, lakini Rais Nkurunziza alisema kuwa Awamu ya kwanza alichaguliwa na Bunge la taifa, hakuchaguliwa na wananchi kwahiyo hakwenda kinyume na katiba ya nchi.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments