Burundi : utawala waionya AU dhidi ya kupelekwa kwa majeshi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amezungumza Jumatano asubuhi kwenye redio ya taifa wakati ambapo amekua akijibu maswali ya waandishi wa habari nchini humo na raia.

Pierre Nkurunziza amedai kuwa nchi yake itakabiliana na askari wa Umoja wa Afrika ambao watatumwa nchini humo. Umoja wa Afrika unajianda kupeleka ujumbe wa kulinda amani nchini Burundi. Itakuchukuliwa "kama mashambulizi" kulingana na rais wa Burundi.

"Azimio lililochukuliwa (na Umoja wa Mataifa) halithibitishi kupelekwa kwa askari nchini Burundi na haiwezekani kupeleka askari nchini Burundi bila ridhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Azimio hilo linabaini kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu uhuru wa Burundi na mipaka yake. Kila mtu anapaswa kuheshimu mipaka ya Burundi.

Kama watakuja wakikiuka azimio hili, watakua wameishambulia nchi ya Burundi na kila raia wa Burundi atasimama kwa ajili ya kupambana. Nchi itakuwa imeshambuliwa na sisi tutajihami kwa kupambana nao", amesema rais Pierre Nkurunziza.

Kwa upande wake, Umoja wa Afrika umewatishia wadau katika mgogoro wa Burundi. Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, katika taarifa iliyotolewa Jumatano hii asubuhi, ametisha kuchukua vikwazo kwa "wale wote ambao watasababisha mazungumzo kuvunjika" na pia "kukataa kuitikia mwaliko wa mpatanishi".

Baada ya kuanza rasmi upatanishi wa Uganda Jumatatu wiki hii, tarehe mpya ya mkutano mwengine imepangwa Januari 6 mjini Arusha nchini Tanzania. Lakini serikali ya Bujumbura mara moja ilisema kuwa hapakua na makubaliano juu ya tarehe hiyo.

RFI Kiswahili

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments