Mchungaji Jean Uwinkindi ahukumiwa kufungwa maisha jela

Jean Uwinkindi aliyekuwa mchungaji wa kanisa la kikristo wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi amehukumiwa na mahaka kuu ya Rwanda kifungo cha maisha jela.

Uwinkindi alikuwa akituhumiwa mauaji ya kimbari ya watu wa kabila la watutsi waliokuwa wamekimbilia katika kanisa lake wilayani Bugesera ya sasa, pamoja na uhalifu dhidhi ya binadamu.

Mchungaji huyu wa zamani ameonekana na hatia ya kuwapa msaada makundi ya wauaji waliokwendea kuwaua watutsi waliokuwa wamekimbilia kanisani, kuwagharamia chakula na vinywaji pia na kuhudhuria mikutano iliyopanga mbinu za kuwaangamiza watutsi.

Mahakama yameongeza kuwa adhabu ya Uwinkindi haiwezi kufupishwa kutokana na unyama uliotumiwa kuwaua marehemu hao na kama mtu aliyejulikana kama muamini pia mchungaji .

Uwinkindi alipelekwa Rwanda na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) baada ya kukamatiwa nchini Uganda mwaka 2010.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments