CHAN 2016 : Uganda yajiandaa kumenyana na Gabon pamoja na Cameroon

Mara baada ya kutoka kwenye mapumziko, kocha wa timu ya taifa ya Uganda Miltuni Sredojević Micho, amesema atatangaza kikosi cha wachezaji 30 cha timu ya Cranes leo jumatano ambapo atachagua wachezaji 24 watakaojipima katika mchezo wa kirafiki na Gabon.

Timu ya taifa ya Gabon iko kwenye kundi la kwanza na Rwanda katika mashindano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN ( African Nations Championship)

Mtanange huo wa kirafiki, Uganda Cranes itacheza tarehe 10 Januari, vile vile wana mpango wa kucheza na Cameroun katika kundi la pili tarehe 13 Januari 2016, michuano yote itafanyika katika uwanja wa Njeru Technical Center mjini Jinja.

Akiongea na gazeti la Daily Monitor, Kocha Milutini amesema vijana waliocheza michuano ya kombe la CECAFA mwaka huu na kuilaza Rwanda kwa bao 1-0 kwenye fainali mjini Adis Abbaba, Ethiopia, hataraji kuwatumia wote, amebaini kuwa Cecafa imemalizika , atatoa nafasi kwa wachezaji wote watakoitwa hii leo halafu atachunguza kwa makini watakaofanya vema, ndio watawakilisha taifa la Uganda.

Inatarajiwa kwamba kocha huyo atatangaza rasmi kikosi kitakachukuja nchini Rwanda kwenye mashindano ya CHAN tarehe 7 Januari 2016.

Uganda Cranes, imeshiriki mara mbili mashindano ya CHAN lakini huondolewa kwenye makundi mapema, imepangwa kwenye kundi D mjini Gisenyi , wilayani Rubavu ambapo itachezea kwenye uwanja wa Umuganda itakuwa pamoja na Zimbabwe, Zambia na Mali.

Mechi ya kwanza itacheza na Mali tarehe 19 januari, mechi ya pili itakuwa pamoja na Zambia tarehe 23 wakati mechi yake ya mwisho itachuana na Zimbabwe tarehe 27 januari 2016.

Mashindano ya CHAN mwaka huu yanataraji kuanza January 17 hadi tarehe 7 Februari 2016.

Makundi

Kundi A : Rwanda, Ivory Coast, Morocco, Gabon
Kundi B : DRC, Ethiopia, Cameroon, Angola
Kundi C : Tunisia, Guinea, Niger, Nigeria
Kundi D : Zimbabwe, Zambia, Uganda, Mali

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments