Rwanda yakanusha madai ya kuchelewa kutoa mchango wa EAC.

Katibu wa kudumu katika wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki INNOCENT Safari, amekanusha habari ambazo zilikuwa zimepitishwa katika baadhi ya magazeti zikisema kuwa Rwanda irichelewa kutowa mchango wake katika jumuia ya Afrika mashariki.

Akikanusha madai hayo Bwana Safari, amesema kuwa Rwanda haikuchelewa kutowa nchango wake kama inavyosadikiwa kwani hivi sasa bado tuko mwezi wa Dicemba.

Amebaini kuwa hakuna uchelewaji uliopo hata kidogo, taarifa zilizotolewa ya kwamba nchi tano za jumuiya hiyo, zilichelewa kutoa mchango wake upatao Milioni 30.9 dola za kimarekani katika bajeti na kusababisha uongezeko la madeni katika muungano huo.

Kwa mjibu wa gazeti la ‘’The Citizen’’ pesa ambazo hazijatolewa zingekuwa tayari zimefikishwa kwenye Akaunti ya EAC hapo tarehe 14 Disemba 2015.

Pamoja na kwamba wanajumuia walikuwa wakikumbushwa kutoa mfano bora, lakini haikuwa hivyo. ameendelea kusema kuwa mchango huo hutolewa kwa awamu nne kwahiyo Rwanda inakaribia kutoa mchango wake siku za hivi karibuni katika awamu ya mwisho.

Aidha , Katibu wa kudumu wa EAC Safari ametowa mfano katika nchi 5 za jumuiya hiyo ambapo Burundi ndio inaongoza katika madeni ikifuatwa na Tanzania. Gazeti la The citizen linasema kuwa Rwanda ina deni la milioni 6.3 dola za kimarekani, Burundi milioni 11.2,Tanzania milioni 4.2. Uganda milioni 2.7.

Haya yakiarifiwa katika bajeti ya mwaka 2014/2015 iliyo idhinishwa na EALA mwaka uliopita walikubaliana kutoa milioni 41.9 dora za kimarekani na zingine zipatazo 73.2 zitakazo tolewa na wahisani.

Bagabo John

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments