MAKALA YA MWAKA 2015 Rais wa Rwanda Paul...

MAKALA YA MWAKA 2015

Rais wa Rwanda Paul Kagame mwezi octoba , alikamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Uholanzi.

Mara baada ya kufanya mkutano na wanyarwanda zaidi ya elfu nne waliohudhuria Rwanda Day iliyopita mjini Amsterdam, Rais Kagame alianza ziara ya kikazi nchini humo ambapo aliongea na mfalme Willem-Alexande pamoja na Queen Máxima kuhusu sekta ya biashara.

Rais Kagame pia alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa baraza la seneti la Uholanzi Ankie Broekers-Knol pia spika wa baraza la bunge Anouchka van Miltenburg na waziri wa mambo ya nchi za nje Mr Bert Koenders.

Akiongea na mwenyekiti wa baraza la seneti, Rais Kagame alisisitiza uhusiano kati ya mataifa mawili.
Alisema : “Ujenzi wa nchi ulitoka mbali. Nashukuru uvumilivu wa wanyarwanda na washirika wao wa uholanzi. Rwanda iliendelea kupiga hatua miaka 20 iliyopita pamoja na kwamba ilipitia wakati mgumu sana’’.

Rais Kagame amewaasa wawekezaji wa Uholanzi kuwekeza mali zao nchini Rwanda.
Kagame akiongea na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uholanzi
Alisema : “ Kuwekeza mali nchini Rwanda siyo faida ya mwekezaji tu bali huwafikia hata watu wa kawaida kubadili hali ya maisha yao’’
Rais Kagame akiongea na mwenyekiti wa Baraza la seneti na spika wa baraza la bunge la Uholanzi . Uholanzi ni moja ya mataifa yaliyoisaidia Rwanda baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwezi April 1994 hadi leo.
Taifa hilo la Uholanzi lilisaidia Rwanda kuhusiana na sekta ya sheria, kilimo na kudhibiti maji.

Mpaka sasa nchini Rwanda kuna miradi 10 ya waholanzi yenye thamani ya milioni 52, 7 ya dola za kimarekani.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na kiwanda cha Heineken , kampuni ya ndege KLM, miradi ya nishati, kilimo na ufugaji.

Rwanda ilifurahia uamuzi wa kutotoa hati ya kuwatia mbaroni wanajeshi wake

Serikali ya Rwanda mwaka huu ilitangaza kufurahia uamuzi wa mahakama ya juu nchini Hispania ya kutozipa thamani hati za kuwatia mbaroni maafisa wakuu wa kijeshi 40 wa Rwanda.

Kwa mujibu wa waziri Leta Johnston Busingye, Waziri wa sheria nchini Rwanda Johnstone Busingye amesema kuwa kesi hizo dhidi ya wanajeshi ni za uongo,zenye msukumo wa kisiasa na na unyanyasaji wa haki zao.

Mahakama ya juu nchini Uhispania imefutilia mbali kesi dhidi ya wanajeshi hao walioshtakiwa mwaka 2008 kwa mashtaka yaliodaiwa kutekelezwa baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mwaka 1994,kulingana na wakili anayewakilisha baadhi ya waathiriwa.

Mahakama ya juu yapinga shtaka la Chama cha kijani

Mwenyekiti wa chama cha Kijani Rwanda Frank Habineza.

Chama cha kijani nchini Rwanda mwaka huu kilitangaza kwamba kitafanya kila liwezekanalo ili katiba ya Rwanda hususan kipengele chake cha 101 na 193 kisibidilishwe.

Chama hicho Green Party kilishtaki serikali kuwa ina mpango wa kubadili katiba kwenye kipengele chake cha 101 na kusema kuwa idadi ya mihura ya rais anayopewa ni kinyume na sheria.

Ameongeza kuwa kuna hatua muhimu zinazofuatwa kuhakikisha katiba haikiukwi
Hata hivyo Jaji Mkuu Sam Rugege amesema katika uamuzi wake katika mahakama hiyo mjini Kigali kwamba mahakama imegundua kuwa kipengee nambari 193 cha katiba hiyo inaruhusu kipengee cha 101 kubadilishwa iwapo hilo litafanywa na wananchi kupitia kura ya maoni.

Mahakama ya juu nchini Rwanda imetupilia mbali kesi iliyonuiwa kuzuia rais Paul Kagame kurefusha hatamu yake ya urais kwa zaidi ya mihula miwili iliyokubaliwa kikatiba.

Mahakama hiyo imesema kesi iliyowasilishwa kwake na chama cha Democratic Green Party of Rwanda haikuwa na maana yoyote.

Chama hicho kilitaka kulizuwia bunge kubadilisha kipengele cha katiba nambari 101 kinachosema kwamba rais anapaswa kuchaguliwa kwa muhula wa miaka 7 na kipindi hicho kinapaswa kurefushwa mara moja tu.

"Hakuna sababu yoyote inayopaswa kumfanya mtu kushikilia hatamu ya uongozi katika ofisi ya jamhuri ya Rwanda kwa zaidi ya vipindi viwili," kama inavyosema katiba ya Rwanda.

Tukinyimwa haki yetu mahakamani, tutaandamana” Mwenyekiti wa Chama cha Green Party.

Hicho ni kichwa cha habari Chama cha upinzani cha Mazingira na Demokrasia (Rwanda Democratic Green Party)

Mwaka huu kilikuwa kimeapa kuwa kitafanya maandamano ikiwa shtaka lake lililofikishwa mahakamani kubadili katiba kuhusu kugombea kwa Rais Paul Kagame katika muhula wa tatu litawekwa kando .

Chama cha Green Party kilifikisha shtaka lake katika mahakama kuu ya Rwanda, ambapo kiliomba mahakama hiyo kukataza bunge la Rwanda lisibadili katiba , ili rais Kagama asiruhusiwe kugombea tena uchaguzi wa rais mwaka 2017.

Mwenyekiti wa chama hicho, Dr Frank Habineza aliliimbia gazeti la Makuruki,rw kwamba wanaamini kuwa mahakama kuu itakuwa makini kuchunguza shtaka hilo.

Habineza aliendelea kusema kwamba lazima katiba isirekebishwe kabisa, hasa kipengele cha 101, kinachomzuia rais kugombea awamu zaidi ya mbili.

Hata hivyo, mamilioni ya raia wamefikisha barua zao bungeni wakiomba katiba irekebishwe, ili Kagame awanie muhula mwingine .

Kwa upande wake, Green Party inasema kwamba mahakama ikipotoshwa na uamuzi wake ukawa si wa kuamini, njia zinazoalia si nyingine bali ni maandamano ili kuonyesha kwamba hawafurahii uamuzi huo.
Dr Habineza alisikika hivi karibuni, akisema kwamba bunge likiamua kubadili katiba, chama chake kitafanya kampeni za kuhamasisha raia wapige kula nafasi ya “HAPANA”.
Chama hicho kimelezea kuwa hawatakuwa na wasiwasi, endapo uendeshaji mashtaka utashinda baada ya kuonyesha ushahidi kamili unaoheshimu sheria.

Chama cha Green Party kimeongeza kuwa watakaponyimwa haki yao, watapeleka shtaka lao katika mahakama nyingine kama vile mahakama ya Jamuiya ya Afrika ya Mashariki.

Green Party ni chama pekee nchini Rwanda, kilichothubutu kupinga muhula wa tatu wa rais Kagame, wakati vyama vingine vilionyesha kuwa vinamuunga mkono rais Kagame akiwania muhula mwingine, kutokana na matendo yake makubwa na hatua iliyofikiwa nchini wakati wa utawala wake.

Katika Nyanja ya kisiasa Wanyarwanda waamuwa mustakbali wa rais

Wanyarwanda wamepiga kura

Wanyarwanda kote nchini tarehe 18 Disemba 2015 walishiriki kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, baadhi walifika mapema saa 12 asubuhi wakisubiri zoezi lenyewe kuanza rasmi saa moja asubuhi.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi mapema

Rais wa jamhuri Paul Kagame aliwasili kwenye kituo cha kupigia kura katika kituo cha Rugunga tarafa ya Nyarugenge mjini Kigali majira ya saa tano asubuhi ambapo amepiga kura kama wanywaranda wengine, alikuwa ameambatana na mkewe Bi Jeannette Kagame na mtoto wao Ange Kagame .

Mara baada ya rais kupiga kura, waandishi wa habari walimuuliza ikiwa atahitaji kugombea tena nafasi ya kuongoza nchi baada ya mwaka2017, Rais Kagame kwa kifupi hakuwa na mengi ya kuongea amejibu : ‘’Subirini matokeo ya uchaguzi’’
Bi Jeannette Kagame naye pia alikuwa ameshiriki kupiga kura
Waziri mkuu Anastase Murekezi ,yeye amepigia kura kwenye uwanja mdogo wa Amahoro Remera (Petit stade).

Waziri Murekezi , amesema kwamba kufanyika kwa zoezi la kupiga kura, hii ini ishara ya maombi ya wanyarwanda sasa yamepewa thamani.

Alisisitiza kwamba kamwe serikali ya Rwanda haitorudisha nyuma maombi ya wananchi.

Baada ya siku mbili matokeo rasmi yalitangazwa.

Matokeo

Kati ya wilaya 30 za Rwanda, 27 waliopiga kura ya YEGO yaani Ndiyo, walikuwa juu zaidi ya asilimia 98%, wanyarwanda waishio nje Diaspora baadhi walipiga kura 100%.

Kwa jumla hesabu za kura za muda zilizotangazwa na Prof. Kalisa Mbanda mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ni 98,1 % ya wanyarwanda wote waliopiga kura ya Ndio.

Wanyarwanda waishio katika mataifa ya Canada, UAE, Djibouti na Tanzania walipiga kura zaidi ya 100%.

Wananchi nchini humo walijitokeza kwa wingi kuitikia mwito huo tangu alfajiri na kupanga foleni ya upigaji kura.

Kulikuwa na waangalizi wa ndani ya nchi hiyo ambao wameeleza kwamba kila kitu kimeenda vizuri kama walivyopanga.

Lakini wanadiplomasia kutoka maeneo mbali mbali wametoa wasi wasi wao na kutokuunga mkono hatua hiyo .

Naye rais Kagame hakutaka kuongea na vyombo vya habari mpaka kura hiyo itakapokamilika na wala hajatoa msimamo wake juu ya kugombea muhula wa tatu

Rwanda imelaani sana ripoti ya Human Rights Watch

Shirika la kutetea haki za binadamu HRW (Human Rights Watch ) mwezi septemba 2015 ilitoa ripoti likituhumu serikali ya Rwanda kutoheshimu haki za binadamu kutokana na kutesa watu walioko kituo cha mpito cha Gikondo. (Gikondo Transit Center.)

Kupitia waziri wa sheria Busingye Johnston, Serikali ya Rwanda imesema tuhuma hizo ni uongo mtupu, na kwamba huko Gikondo hakuna gereza.

HRW imesema kuwa gerezani Gikondo, wafungwa huhudumiwa vibaya , kukosa matibabu wakati wa magonjwa, kupewa chakula kisichotosha, kucharazwa na mengineyo.

Ripoti hiyo huonyesha pia kuwa rushwa hujitokeza kwa hao wanaotaka waachiwe huru, kuwa wanawahonga maafisa walinzi wa gereza ili wafungwa hao waone kutoka nje.

HRW imendelea kusema kuwa wanaume wanaombwa rushwa mara mbili kuliko ya wanawake, ili wakubaliwa kuachiwa huru.

Waziri Busingye amesema kuwa ripoti hiyo ni uongo ambao hauna kiini. Amesema kuwa Gikondo si gereza bali Kituo cha mpito kwa hao waliokumbwa na madawa ya kulevya, makahaba na wengine ambao tabia zao hazifanani na mwongozo wa jamii.
Aliendelea kusema kwamba watu hao wanakosolewa kwa muda mfupi, na kufundishwa kazi kama ujengaji, uselemala, kushona na nyinginezo ili waweze kuiishi vema katika jamii.

Mwaka uliopita, serikali ya Rwanda na HRW walikaa pamoja na kukubaliana kuwa hawatatangaza tena ripoti bila kushauriana, kwani ripoti za kwanza tena Rwanda ilikuwa ikizipinga kuwa si ukweli.
Rais Kagame awapa mbinu viongozi wa Burundi kutafuta suluhu

Rais Paul Kagame

Rais Kagame waambia dawa ya kuepuka mauaji ya kimbari wanayo wenyewe wasitegemee nchi jirani.

Kigali, Rwanda. Rais wa Rwanda Paul Kagame amewashauri raia wa Burundi kumaliza mgogoro unaoendelea nchini humo kwani hakuna mtu wa nje anayeweza kufanya hivyo.

Rais Kagame alisema kuwa, viongozi na nchi hiyo na raia hao wana wajibu wa kushughulika na mambo yao ya ndani kuliko kutegemea msaada wa watu wengine.
“Siyo kweli kwamba Rwanda inafurahia mgogoro wa kisiasa unaoendelea Burundi kwani athari zake zinatugusa hata huku. Wakimbizi wanazidi kuongezeka hivyo ni vyema wakatafuta ufumbuzi haraka iwezekanavyo kuyanusuru maisha ya watu,” alisema.

Kiongozi huyo alikanusha uvumi kwamba nchi yake imekuwa ikisaidia baadhi ya makundi ya wapiganaji yanayopingana na Serikali ya Burundi.

“Hayo ni madai ya yasiyo ya kweli na kama kuna mwenye ushahidi kuhusu hilo athibitishe. Huu siyo wakati wa lawama kwani jambo la muhimu ni suluhu itakayomaliza mgogoro huo,” alisema.

Amuunga mkono Museveni

Katika hatua nyingine, Kagame alionyesha kumuunga mkono Rais wa Uganda Yoweri Museveni anayewania madarakani kwa muhula wa tano.

“Ukiniuliza mtazamo wangu kuhusu Uganda jibu ni kwamba nimefanya kazi vizuri na viongozi waliopo madarakani hivyo nawatakia kila la heri kwenye uchaguzi ujao,” alisema na kuongeza kuwa :

“Naamini waganda ni watu wenye akili timamu na uelewa wa kutosha utakaowawezesha kufanya uchaguzi sahihi bila kuleta machafuko katika nchi yao.”
Kuhusu uamuzi ambao mataifa ya magharibi yanaweza kuchukua kutokana na kufanyika mabadiliko Katiba ya Rwanda, Kagame alisema Wanyarwanda hawawezi kuishi kwa kufuata matakwa ya watu wengine.

“Wanyarwanda wataishi wanavyotaka. Hatuwezi kuwa waoga na watiifu kupita kiasi kwa vile tunategemea misaada kutoka kwa wahisani, binafsi sidhani kama kuna matatizo makubwa yanayoweza kutokea na yakawa zaidi ya yaliyowahi kutukuta,” alisema.

Mwaka huu aliyekuwa waziri wa michezo na utamaduni Joseph HABINEZA alisimamishwa kazi baada ya miezi 7. Haya ni baadhi ya mabadiliko ya haraka yaliyotokea kwa kiongozi huyo aliyekuwa amefurahiwa na wengi baada ya kurejea wizarani miaka miwili iyopita.

Balozi Joseph Habineza alirejea nchini akitokea kwenye ubalozi wa Rwanda nchini Nigeria .

Mpaka sasa hakuna sababu rasmi inayofahamika wazi juu ya kufukuzwa kwawe kazini, naye alishangaa hajui sababu , alikanusha habari zisemazo kuwa kufukuzwa kwakwe kumetokana na ufujaji wa pesa ya umma wakati wa uchaguzi wa Miss Rwanda 2015.

Mahakama ya juu yapinga shtaka la Chama cha kijani

Mahakama ya juu nchini Rwanda ilitupilia mbali kesi iliyonuiwa kuzuia rais Paul Kagame kurefusha hatamu yake ya urais kwa zaidi ya mihula miwili iliyokubaliwa kikatiba.

Mahakama hiyo imesema kesi iliyowasilishwa kwake na chama cha Democratic Green Party of Rwanda haikuwa na maana yoyote.

Chama hicho kilitaka kulizuwia bunge kubadilisha kipengele cha katiba nambari 101 kinachosema kwamba rais anapaswa kuchaguliwa kwa muhula wa miaka 7 na kipindi hicho kinapaswa kurefushwa mara moja tu.

"Hakuna sababu yoyote inayopaswa kumfanya mtu kushikilia hatamu ya uongozi katika ofisi ya jamhuri ya Rwanda kwa zaidi ya vipindi viwili," kama inavyosema katiba ya Rwanda.

Tukinyimwa haki yetu mahakamani, tutaandamana” Mwenyekiti wa Chama cha Green Party.

Hicho ni kichwa cha habari Chama cha upinzani cha Mazingira na Demokrasia (Rwanda Democratic Green Party)

Mwaka huu kilikuwa kimeapa kuwa kitafanya maandamano ikiwa shtaka lake lililofikishwa mahakamani kubadili katiba kuhusu kugombea kwa Rais Paul Kagame katika muhula wa tatu litawekwa kando .

Chama cha Green Party kilifikisha shtaka lake katika mahakama kuu ya Rwanda, ambapo kiliomba mahakama hiyo kukataza bunge la Rwanda lisibadili katiba , ili rais Kagama asiruhusiwe kugombea tena uchaguzi wa rais mwaka 2017.

Mwenyekiti wa chama hicho, Dr Frank Habineza amelimbia gazeti la Makuruki,rw kwamba wanaamini kuwa mahakama kuu itakuwa makini kuchunguza shtaka hilo.

Habineza aliendelea kusema kwamba lazima katiba isirekebishwe kabisa, hasa kipengele cha 101, kinachomzuia rais kugombea awamu zaidi ya mbili.
Hata hivyo, mamilioni ya raia wamefikisha barua zao bungeni wakiomba katiba irekebishwe, ili Kagame awanie muhula mwingine .

Kwa upande wake, Green Party inasema kwamba mahakama ikipotoshwa na uamuzi wake ukawa si wa kuamini, njia zinazoalia si nyingine bali ni maandamano ili kuonyesha kwamba hawafurahii uamuzi huo.
Dr Habineza alisikika hivi karibuni, akisema kwamba bunge likiamua kubadili katiba, chama chake kitafanya kampeni za kuhamasisha raia wapige kula nafasi ya “HAPANA”.

Chama hicho kimelezea kuwa hawatakuwa na wasiwasi, endapo uendeshaji mashtaka utashinda baada ya kuonyesha ushahidi kamili unaoheshimu sheria.
Chama cha Green Party kimeongeza kuwa watakaponyimwa haki yao, watapeleka shtaka lao katika mahakama nyingine kama vile mahakama ya Jamuiya ya Afrika ya Mashariki.

Green Party ni chama pekee nchini Rwanda, kilichothubutu kupinga muhula wa tatu wa rais Kagame, wakati vyama vingine vilionyesha kuwa vinamuunga mkono rais Kagame akiwania muhula mwingine, kutokana na matendo yake makubwa na hatua iliyofikiwa nchini wakati wa utawala wake.

Katika Nyanja ya kisiasa vile vile Wanyarwanda waamuwa mustakbali wa rais

Wanyarwanda wamepiga kura

Wanyarwanda kote nchini tarehe 18 Disemba 2015 walishiriki kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, baadhi walifika mapema saa 12 asubuhi wakisubiri zoezi lenyewe kuanza rasmi saa moja asubuhi.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi mapema

Rais wa jamhuri Paul Kagame aliwasili kwenye kituo cha kupigia kura katika kituo cha Rugunga tarafa ya Nyarugenge mjini Kigali majira ya saa tano asubuhi ambapo amepiga kura kama wanywaranda wengine, alikuwa ameambatana na mkewe Bi Jeannette Kagame na mtoto wao Ange Kagame .

Mara baada ya rais kupiga kura, waandishi wa habari wamemuuliza ikiwa atahitaji kugombea tena nafasi ya kuongoza nchi baada ya mwaka2017, Rais Kagame kwa kifupi hakuwa na mengi ya kuongea amejibu : ‘’Subirini matokeo ya uchaguzi’’
Bi Jeannette Kagame naye pia alikuwa ameshiriki kupiga kura
Waziri mkuu Anastase Murekezi ,yeye amepigia kura kwenye uwanja mdogo wa Amahoro Remera (Petit stade).

Waziri Murekezi , amesema kwamba kufanyika kwa zoezi la kupiga kura, hii ini ishara ya maombi ya wanyarwanda sasa yamepewa thamani.
Alisisitiza kwamba kamwe serikali ya Rwanda haitorudisha nyuma maombi ya wananchi.

Baada ya siku mbili matokeo rasmi yalitangazwa.

Matokeo

Kati ya wilaya 30 za Rwanda, 27 waliopiga kura ya YEGO yaani Ndiyo, walikuwa juu zaidi ya asilimia 98%, wanyarwanda waishio nje Diaspora baadhi walipiga kura 100%.

Kwa jumla hesabu za kura za muda zilizotangazwa na Prof. Kalisa Mbanda mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ni 98,1 % ya wanyarwanda wote waliopiga kura ya Ndio.

Wanyarwanda waishio katika mataifa ya Canada, UAE, Djibouti na Tanzania walipiga kura zaidi ya 100%.

Wananchi nchini humo walijitokeza kwa wingi kuitikia mwito huo tangu alfajiri na kupanga foleni ya upigaji kura.

Kulikuwa na waangalizi wa ndani ya nchi hiyo ambao wameeleza kwamba kila kitu kimeenda vizuri kama walivyopanga.

Lakini wanadiplomasia kutoka maeneo mbali mbali wametoa wasi wasi wao na kutokuunga mkono hatua hiyo .
Naye rais Kagame hakutaka kuongea na vyombo vya habari mpaka kura hiyo itakapokamilika na wala hajatoa msimamo wake juu ya kugombea muhula wa tatu

Rwanda imelaani sana ripoti ya Human Rights Watch

Shirika la kutetea haki za binadamu HRW (Human Rights Watch ) mwezi septemba 2015 ilitoa ripoti likituhumu serikali ya Rwanda kutoheshimu haki za binadamu kutokana na kutesa watu walioko kituo cha mpito cha Gikondo. (Gikondo Transit Center.)

Kupitia waziri wa sheria Busingye Johnston, Serikali ya Rwanda imesema tuhuma hizo ni uongo mtupu, na kwamba huko Gikondo hakuna gereza.

HRW imesema kuwa gerezani Gikondo, wafungwa huhudumiwa vibaya , kukosa matibabu wakati wa magonjwa, kupewa chakula kisichotosha, kucharazwa na mengineyo.

Ripoti hiyo huonyesha pia kuwa rushwa hujitokeza kwa hao wanaotaka waachiwe huru, kuwa wanawahonga maafisa walinzi wa gereza ili wafungwa hao waone kutoka nje.

HRW imendelea kusema kuwa wanaume wanaombwa rushwa mara mbili kuliko ya wanawake, ili wakubaliwa kuachiwa huru.
Waziri Busingye amesema kuwa ripoti hiyo ni uongo ambao hauna kiini. Amesema kuwa Gikondo si gereza bali Kituo cha mpito kwa hao waliokumbwa na madawa ya kulevya, makahaba na wengine ambao tabia zao hazifanani na mwongozo wa jamii.
Aliendelea kusema kwamba watu hao wanakosolewa kwa muda mfupi, na kufundishwa kazi kama ujengaji, uselemala, kushona na nyinginezo ili waweze kuiishi vema katika jamii.

Mwaka uliopita, serikali ya Rwanda na HRW walikaa pamoja na kukubaliana kuwa hawatatangaza tena ripoti bila kushauriana, kwani ripoti za kwanza tena Rwanda ilikuwa ikizipinga kuwa si ukweli.

Kwa kifupi hizo ni baadhi ya habari muhimu za kisiasa zilizojili mwaka huu, nawatakieni kila la kheri na mafanikio ya mwaka mpya wa 2016.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments