Polisi yaahidi kuwarejesha walevi wakati wa sikuu kuu za mwishoni mwa mwaka


ACP Twahirwa Celestin, msemaji wa Polisi wa Rwanda

Jeshi la Polisi la Rwanda, kama ilivyofanya mwaka jana, imekubali kuwa itawarejesha walevi na wengine wote nyumbani watakao kuwa na tatizo la usalama mdogo katika sikuu kuu za mwishoni mwa mwaka.

Akizungumza na makuruki.rw, msemaji wa Polisi ya Rwanda ACP Cestin, amewatakia wanyarwanda siku kuu njema za mwishoni mwa mwaka, hata hivyo
amewakumbusha wanyarwanda kwamba atakaye kuwa na tatizo au kuwa dhaifu kutokana na kunywa pombe kuzidi kiasi, anaweza kuomba walinda usalama na kumsaidia kumpeleka nyumbani.

ACP Celestin Twahirwa, ameongeza kwamba siku za mwishoni mwa mwaka utakuta watu wanafurahi kupita kiasi, baadhi yao wanaleta vurugu. Amewatolea wito kuwa wataoleta fujo polisi iko chonjo kudhibiti usalama wa raia.
Aidha, ACP Twahirwa ametangaza kuwa mwishoni mwa mwaka uliopita khakuna makosa ya hali ya juu yaliyojitokeza nchini.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments