Magufuli amfuta kazi afisa mkuu wa reli


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni ya reli Tanzania (RAHCO) Benhadard Tito
.

Mhandisi Tito amelazimishwa kukaa kando ili kufanikisha uchunguzi katika utaratibu uliotumika wakati wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Magufuli alichukua hatua hiyo kali baada ya mkutano na wadau wanaohusika na ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”

Uchunguzi wa kimsingi unaelekezwa kwa utoaji wa zabuni hiyo inayokisiwa kugharimu takriban dola milioni $14.

.
Sasa Magufuli al maarufu "The Bulldozer" ameiagiza mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.

Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments