Amnesty yainyooshea kidole Burundi

Shirika la kutetea haki za Binadamu Ulimwenguni la Amnesty International,limeituhumu serikali ya Burundi kwa mauaji watu wasio na hatia na matumizi mabaya ya jeshi la nchi hiyo.

Shirika hilo limelaani mauaji yaliyotokea Desemba 11 ambapo watu zaidi ya 70 waliuawa wakati jeshi la serikali lilipokuwa likijihami dhidi ya mashambulizi ya waasi waliovamia vituo vitatu tofauti vya jeshi.

Serikali ya Burundi iliwaelezea wale waliouawa kuwa ni maadui,jambo ambalo linapingwa vikali na Amnesty ambao wanasema kuwa wengi wa waliouawa ni watu wasio na hatia na raia wa taifa hilo.

Ripoti ya shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.

shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.

Kutokana na hali hiyo Umoja wa Afrika AU unasisitiza baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha mpango wake wa kupeleka kikosi cha wanajeshi 5000 wa kulinda amani nchini kufuatia mauaji ya raiayanayoendelea.

Hata hivyo serikali ya Burundi inapinga hatua hiyo.

Wabunge nchini Burundi wameanza mjadala kuhusu hatua ya muungano ya Afrika wa kutuma kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 cha kulinda amani nchini humo, hatua ambayo inafaa kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Hatua hiyo imepingwa vikali na serikali ya rais Pierre Nkurunziza, ikitaja kikosi hicho kuwa cha kigeni kinachovamia taifa hilo.

Kufuatia msimamo wa bunge la nchi hiyo kukataa majeshi ya muungano huo

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments