Rais Kagame apongeza vijana walivyoitikia kura ya maoni


Rais wa jamhuri Paul Kagame, amepongeza vijana jinsi walivyoitikia kwa wingi katika zoezi la upigaji wa kura ya maoni. Amebaini kuwa inatoa ishara nzuri kwa kizazi kijacho ambapo wazazi wao walichokipigania wameeanza kukifikia.

Haya mkuu wa nchi, ameyasema wakati wa kufugua rasmi mdahalo wa 13 unaofanyika mjini Kigali ambao umewaleta kwa pamoja watu zaidi ya 1000 wakiwemo viongozi kutoka ngazi za mwanzo, viongozi wa ngazi za usalama, za kisiasa, wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, mabalozi, wanyarwanda waishio ng’ambo na marafiki wa Rwanda.

Rais Kagame amewapongeza kwa jumla wananchi waliopiga kura ya Ndiyo na hapana ili watoe fikra zao kwa mabadiliko ya kura ya maoni ili kubadili katiba ya taifa nchini Rwanda.

Kuhusu watu wanaopotoshwa na kutukanana huku wakipinga sra za nchi, Rais Kagame, amesema : ‘’ Rwanda hakuna tatizo lolote kwa watu wanaokosoa mambo kadhaa yanayotendeka nchini kwani baadhi ya mambo yanayoweza kukosolewa na kuleta faida katika maendeleo ya nchi, lakini nalaani wale wanaotutukana kiwazi na kupinga sera za wanyarwanda zilizofikiwa’’.

Rais Kagame, amesema kwamba Rwanda haina tatizo lolote kwa watu wanaounga mkono na kutoa fikra zao katika ujenzi wa taifa au wanaokosoa mambo kwani yanaweza kuwa na manufaa lakini amepuuzia sana wanaosema kuwa eti Rwanda hawawezi kufikia chochote.

Rais Kagame amewashukuru wanaounga mkono sera za nchi

Rais wa jamhuri ameendelea kusema kwamba kuna mengi ya kufurahia ambapo inayoonyesha wazi hatua Rwanda iyofikia sasa na mahali ilikotokea.

Ni kwa matinki hiyo wanyarwanda wanajiandaa kutoa mchango wao wa kulinda yaliyofikiwa.
Amesema : ‘’ Rwanda tuliyonayo, ni tofauti ni le ya miaka 20 iliyopita . Tunajua pia thamani ya katiba ya taifa, tunajiandaa kulinda hadhi yetu, tutaendelea kuwa na sauti moja’’.

Rais Kagame, amesema kwamba Rwanda ya kesho iko mikononi mwao wenyewe

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments