Wanyarwanda waamuwa mustakbal wa rais

Kati ya wilaya 30 za Rwanda, 27 waliopiga kura ya YEGO yaani ndio walikuwa juu zaidi ya asilimia 98%, mataifa ya nje ambako kuna wanyarwanda Diaspora kuna baadhi walipiga kura 100%

Kwa jumla hesabu za kura za muda zilizotangazwa na Prof. Kalisa Mbanda mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ni 98,1 % ya wanyarwanda wote waliopiga kura ya Ndio.

Wanyarwanda waishio katika mataifa ya Canada, UAE, Djibouti na Tanzania walipiga kura zaidi ya 100%.

Wananchi nchini humo walijitokeza kwa wingi kuitikia mwito huo tangu alfajiri na kupanga foleni ya upigaji kura.

Kulikuwa na waangalizi wa ndani ya nchi hiyo ambao wameeleza kwamba kila kitu kimeenda vizuri kama walivyopanga.

Lakini wanadiplomasia kutoka maeneo mbali mbali wametoa wasi wasi wao na kutokuunga mkono hatua hiyo .

Naye rais Kagame hakutaka kuongea na vyombo vya habari mpaka kura hiyo itakapokamilika na wala hajatoa msimamo wake juu ya kugombea muhula wa tatu.

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments