Raia wa Rwanda walio ng’ambo wapiga kura

Leo tarehe 17 Disemba 2015, wanyarwanda wanoishi nchi za kigeni wamepiga kura (referendum)

Hata hivyo badhi ya wanyarwanda wamesema kwamba hawakushiriki katika zoezi la uchaguzi kutokana kwamba wamenyimwa ruhusa.

Wanyarwanda waishio nchini Sweden, wamesema kwamba zoezi la uchaguzi limefanyika vizuri, polisi wa nchi hiyo wamelinda usalama wao.
Baadhi ya Wanyarwanda wengine wamefanya zoezi hilo katika mataifa ya
Scandinavia, Sweden, Norway na Denmark.
Kwa upande wa bara la Afrika , wanyarwanda wamejiandaa kufanya uchaguzi vizuri
.
Tarehe 19 Disemba tume ya taifa ya uchaguzi itatangaza matokeo ya muda ya uchaguzi na baada ya siku mbili matokeo yatatangazwa rasmi.

Uchaguzi wa “Referendum” yana lenga kuwapa nafasi wananchi wajiamlie kubadili baadhi ya vipengele vya katiba ya Rwanda kwani wao ndio waliomba kuwepo mabadiliko.

Christopher Karenzi
.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments