TP Mazembe washindwa tena Japan Mabingwa wa...

TP Mazembe washindwa tena Japan

Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamecharazwa 2-1 na Club America ya Mexico katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu.

Mechi hiyo ilikuwa ya kuamua nani angemaliza nambari tano katika fainali hizo ambazo zinachezewa Japan.

Dario Benedetto na Martin Zuniga walifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuwaweka mabingwa hao wa Concacaf kwenye udhibiti wa mechi hiyo.

Rainford Kalaba alikombolea mabingwa wa Afrika mechi moja zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kuisha.

 TP Mazembe yachapwa 3-0 Klabu Bingwa Duniani
 Samatta katika orodha ya 3 bora ya CAF
 Samatta, kijana anayevumisha soka ya Tanzania

Lakini mabingwa hao hawakuweza kujikwamua na safari yao kwenye michuano hayo iliisha kwa masikitiko.

Kabla ya mechi hiyo, Mazembe walikuwa wamechapwa 3-0 na Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan hatua ya robofainali, kwenye mechi iliyochezewa mjini Osaka Jumapili.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments