EALASCA, vikombe vingi vilibaki nchini Rwanda

Mashindano ya EALASCA, (East African Local Authorities Sports and Culture Associations) yaliyokuwa yakifanyika mjini Kigali yalifikia kilele chake ijumaa tarehe 11 Disemba 2015

Timu mbali zilizoshiriki ni kutoka nchini Kenya, Uganda na mwenyeji Rwanda. Burundi na Tanzania hazikushiriki.

Mashindano hayo yaliyomaliza wiki nzima, Rwanda ndiyo iliibuka na ushindi wa kutwaa vikombe vingi na medali. Kwa jumla ilijizolea vikombe 8, Uganda vikombe 5 huku Kenya ikiondoka na vikombe 2.

Kwa kifupi timu ya soka ya halmashauri ya jiji la Kigali iliondoka na ushindi na kutwaa kombe , Uganda ya pili na Kenya ikawa ya tatu.

Pool table Rwanda ni mabingwa wakifuatwa na Kenya hatimaye nafasi ya tatu ni Uganda.

Darts Kenya iliibuka na ushindi,na kutwaa kombe, nafasi ya pili Rwanda wa tatu ni Uganda.

Net ball wanawake : Huu mchezo unachezwa na timu za wanawake tu. Rwanda bado ina safari ndefu kucheza michuano ya Net ball

1 Uganda
2 Rwanda
3 Kenya

Volley ball wanaume

1 Rwanda
2 Kenya
3 Uganda

Volley ball wanawake

1 Rwanda
2 Uganda
3 Kenya

Riadha wanaume

1 Uganda
2 Rwanda
3 Kenya

Riadha Wanawake

1 Uganda
2 Rwanda
3 Kenya

Basket ball

1 Rwanda
2 Uganda
3 Kenya haikuwakilisha timu yao

Michezo ya kitamaduni

1 Uganda iliongoza kwa alama nyingi
2 Rwanda
3 Kenya

Mchezo wa kitamaduni mchanganyiko ( kuiga mtindo wa Afrika ya mashariki)

1Rwanda iliibuka na ushindi
2Uganda
3Kenya

Nyimbo

1Uganda iliongoza ilitumia muda wake vizuri
2 Rwanda
3 Kenya

Wataalamu wa kucheza na kuimba hususan wamasai hawakushiriki mashindano.
Katika shughuli za pamoja (Umuganda)

1.Uganda ilitwaa kombe, siri si nyingine bali walitoka Kampala wakiwa wamejiandaa vilivyo, siku ya umuganda baadhi ya waganda walikuwa wamevalia nguo mahsusi ya kazi na mara bada ya kufika tarafani Masaka katika wilaya ya Kicukilo, walichapa kazi wakiwa pamoja na wakenya na wanyarwanda
2.Rwanda ilishikilia nafasi ya pili
3.Kenya

Mashindano ya EALASCA mwakani yatafanyika nchini Kenya jijini Nairobi.
Kenya iliondoka pia na kombe la fair play.

Kwa ujumla Rwanda ilitawazwa kombe kama mwenyeji na mwandalizi wa mashindano (Overall)

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments